Katibu
Mkuu wa Chama cha ACT - Wazalendo, Samson Mwigamba amejiuzulu nafasi
yake ili apate nafasi ya kwenda masomoni Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini
Kenya.
Kwa
mujibu wa ACT-Wazalendo, kamati ya uongozi imekubali maombi ya Mwigamba
na kumruhusu kwenda masomoni na kuwa mchakato wa kujaza nafasi hiyo
utaanza mara moja.
Naye
Mwigamba ameushukuru uongozi wa chama chake kwa ushirikiano waliompatia
tangu chama hicho kinaanzishwa. Amesisitiza kwamba bado ni mwanachama
na ataendelea kutoa ushirikiano hata akiwa nje ya nchi.
Mwanasiasa
huyo anakwenda kusoma shahada ya uzamili katika masuala ya utawala na
usimamizi wa biashara (MBA) na baada ya masomo hayo ataendelea na
shahada ya uzamivu (PhD).
Post a Comment