Msafara wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jafo leo asubuhi ulipotea njia kutokana na watumishi wa Manispaa ya Dodoma kutojua eneo ambalo waziri huyo alikuwa analitembelea.
Waziri Jafo
alikuwa amepanga kufanya ziara kwenye Shule ya Msingi ya Nzuguni B kwa
lengo la kuangalia mapungufu, hasa tatizo la uhaba wa madawati, lakini
hakufika kama alivyotarajia kutokana na watumishi hao kutojua eneo
ambalo shule hiyo iko.
Shule hiyo haijawahi kutembelewa na ofisa elimu tangu mwaka 2007 licha ya kuwa kilomita 6 kutoka katikati ya mji.
Naibu
Waziri alikasirishwa na kitendo hicho akawataka watumishi wa idara ya
Elimu wajipime kama wanastahili kuendelea kufanya kazi.
“Mstahiki Meya, mimi niliona wazi kuwa watumishi wako wananipoteza," alisema Waziri Jafo.
"Nimechukia
sana na hawa watu. Tatizo lao ni kwamba hawajawahi kuja katika shule
hii tangu mwaka 2007, lakini wamekaa ofisini tu. Ikiwezekana waondolewe
na kupelekwa vijijini,” alisema Jafo.
Post a Comment