Watu
wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi
helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la maswa lililoko
wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti
na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.
Kufuatia
tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe
amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa
kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama
inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa
maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa na kwa
uhifadhi wa taifa la Tanzania.
Waziri
Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo ilipotunguliwa na kuikuta
helkopita hiyo iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia wa
Uingereza ambae alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio
hilo limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe
haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya
baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana
na wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.
Nae
kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio
hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada
ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori hilo ambapo Tembo
watatu waliuwawa na kwamba watu watatu wanashikiliwa na polisi
wakihojiwa kufuatia tukio hilo.
==> Hili
ni tukio la kwanza katika historia ya uhifadhi nchini mwetu kwa
Majangili kumpiga risasi na kumuua Rubani na kisha kuangusha helikopta
.
==>Kepten
Roger alikuwa akienda kuongeza nguvu ya askari wa uhifadhi waliokuwa
wakipambana na majangili hatari wilayani Meatu, Simiyu katika ranchi ya
wanyamapori ya Mwiba.
Post a Comment