Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji
Makao Makuu Dodoma (CDA).
Taarifa
iliyotolewa jana tarehe 20 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Paskasi Muragili umeanzia
tarehe 17 Februari, 2016.
Kabla
ya Uteuzi huo Mhandisi Paskasi Muragili alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), nafasi aliyoichukua
kuanzia mwaka 2012.
Post a Comment