Mbunge
wa Arumeru Mashariki, Gibson Ole Maiseyeki (Chadema) amesema bei ya
maziwa nchini ni ndogo kuliko ya maji, hivyo kuitaka Serikali kupanga
bei elekezi ya bidhaa hiyo ili kuleta tija kwa wafugaji.
Maiseyeki alisema Tanzania ni nchi ambayo wafugaji huuza maziwa kwa bei ndogo, kuliko nchi nyingine duniani.
“Ni lini Serikali itakuja na bei elekezi ya maziwa, ili kuipa tija sekta ya wafugaji nchini?” alihoji Maiseyeki.
Akijibu
swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha
alisema bei ya bidhaa mbalimbali zinatokana na nguvu ya soko.
Katika
swali la msingi, Maiseyeki alitaka kufahamu jitihada za makusudi za
Serikali kuwatafutia wafugaji mbegu bora za mifugo, huku akiwasambazia
kwa bei nafuu ili kuondokana na aina ya mifugo ambayo haina tija.
Ole
Nasha alisema Serikali inajitahidi kuhakikisha wafugaji wanapata mbegu
bora za mifugo kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwamo uhawilishaji.
Post a Comment