Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, imeanza zoezi la kupanga shule katika makundi ili kuweka viwango vya ada kwa kuzingatia ubora wa huduma na kwamba haitaathiri ubora wa elimu.
Naibu Waziri wa
wizara hiyo, Stella Manyanya, aliyasema hayo wakati akijibu swali la
msingi la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema).
Mdee alitaka kufahamu iwapo Serikali imebaini kiwango cha gharama kwa kila mwanafunzi kwa shule za bweni na kutwa, iwapo hakitasababisha kuporomoka kwa ubora wa elimu.
Mdee alitaka kufahamu iwapo Serikali imebaini kiwango cha gharama kwa kila mwanafunzi kwa shule za bweni na kutwa, iwapo hakitasababisha kuporomoka kwa ubora wa elimu.
Manyanya alisema wizara hiyo imefanya utafiti kuhusu
gharama za kila mwanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari.
“Baada ya utafiti, wizara yangu ilifanya mazungumzo na baadhi ya taasisi zinazosimamia elimu kwa shule zisizokuwa za Serikali na kukubaliana jinsi ya kufikia viwango vya ada elekezi,” alisema.
“Baada ya utafiti, wizara yangu ilifanya mazungumzo na baadhi ya taasisi zinazosimamia elimu kwa shule zisizokuwa za Serikali na kukubaliana jinsi ya kufikia viwango vya ada elekezi,” alisema.
Alisema
wizara inatarajia ubora wa ada elekezi hautaathiri elimu kwa shule
binafsi, kwa sababu itapangwa kulingana na ubora wa miundombinu ya
shule.
Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan
Lyimo (Chadema) alitaka kufahamu jinsi Serikali inavyotaka kupanga bei
elekezi wakati imeifanya elimu kuwa biashara.
Manyanya alisema
siyo mara ya kwanza kwa Serikali kupanga bei elekezi kwa faida ya
wananchi na kwamba, imefanyika kwa upande wa huduma ya maji hivyo
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura) wamefanya.
Post a Comment