Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) mwishoni mwa wiki
imesaini mkataba na Kampuni ya CreditInfo Tanzania Ltd utakaowezesha
taarifa za wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kufikishwa katika Kitengo
Uratibu za Taarifa za Mikopo (Credit Reference Bureau) kilichopo katika
Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kampuni ya CreditInfo Ltd ina leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Hivyo
basi, mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu ambaye ataomba mkopo kutoka
kwenye taasisi yoyote ya kifedha hapa nchini, taasisi hiyo itakuwa na
uwezo wa kuhakiki kama mwombaji huyo ni munufaika wa mkopo wa elimu ya
juu na ikiwa ana nidhamu ya kurejesha mikopo.
Kwa
mujibu wa mkataba huo, HESLB itawasilisha orodha ya wadaiwa wa mikopo
ya elimu ya juu kwa kampuni ya CreditInfo ambayo itahakikisha taarifa za
wakopaji zinapatikana kwa taasisi zote za kifedha, yakiwemo mabenki,
ili taasisi hizo zijiridhishe kabla ya kutoa mikopo mipya kwa wanufaika
wa mikopo ya elimu ya juu.
“HESLB
ina furaha kufanya kazi na CreditInfo kama mdau mpya. Tunawasihi
wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu waanze kulipa madeni yao ili wawe na
hadhi ya kukopesheka na taasisi za kifedha,” alisema
kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi wakati wa hafla fupi
ya kutia saini mkataba huo katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Kwa
upande wake, Mtendaji Mkuu wa CreditInfo Tanzania Ltd Bw. Davith Kahwa
amesema lengo la kampuni yake ni kuhakikisha fursa za ukopaji
zinazongezeka na wakopaji wanakuwa na nidhamu kwa mikopo waliyopata.
“Wanufaika
wa mikopo ya elimu ya juu ambao wamekuwa wakilipa watapata fursa ya
kipekee ya kujadiliana na taasisi za kifedha kuhusu viwango vya riba kwa
sababu ya nidhamu wanayoionyesha kwa mikopo yao,” alisema Bw. Kahwa katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Meneja wa CreditInfo Tanzania Bw. Van Reynders.
”Tumedhamiria kuiunga mkono HESLB katika kutekeleza majukumu yake hususan yale ya ukusanyaji mikopo iliyoiva,” aliongeza Mtendaji Mkuu huyo wa CreditInfo Tanzania Ltd.
HESLB
ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi
Julai 2005 ili kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji na pia kukusanya
mikopo iliyoiva ambayo imekuwa ikitolewa na Serikali tangu mwaka 1994.
Hadi
sasa, zaidi ya Tshs 2.1 trilioni zimetolewa kwa watanzania na, kati ya
hizo, Tshs 258 bilioni zimeiva na hivyo kutakiwa kukusanywa kutoka kwa
wanufaika.
Kiasi kilichobaki kinajumuisha fedha walizopewa wanafunzi ambao bado wanaendelea na masomo na ambao muda wa kuanza kuwadai (miezi 12 baada ya kumaliza masomo) haujafika.
Kiasi kilichobaki kinajumuisha fedha walizopewa wanafunzi ambao bado wanaendelea na masomo na ambao muda wa kuanza kuwadai (miezi 12 baada ya kumaliza masomo) haujafika.
CreditInfo
Tanzania Ltd ni sehemu ya Kampuni ya Kimataifa inayofanya kazi kwenye
nchi zaidi ya 20 duniai na inayojishughulisha na usimamizi wa taarifa za
mikopo. Ilisajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2013.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
(HESLB) Bw. Jerry Sabi (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
CreditInfo Tanzania Ltd Bw. Davith Kahwa wakisaini mkataba ambao
utaiziwezesha taasisi za kifedha zinazotoa mikopo nchini kuhakiki
taarifa za waombaji mikopo, ambao ni wanufaika wa mikopo ya elimu ya
juu, kabla ya kuwapa mikopo mipya. Wengine ni Bw. Frimat Tarimo,
Mwanasheria wa HESLB na Bw. Van Reynders, Meneja wa CreditInfo Tanzania.
(Picha: HESLB).
Post a Comment