Saturday, 9 April 2016
Kipini cha puani cha DiamondChageuka kuwa Gumzo mitaani
Posted by Unknown on 07:50:00 in | Comments : 0
Watu wanahofia kipini cha pua cha Diamond kuliko hata kesho yao.
Kinachowaumiza zaidi mashabiki wake ni kuwa haoneshi kujali kilio chao. Aliwashtua sana juzi pale alipoweka picha ikimuonesha akiwa na kipini hicho na wengi walihisi amejitoga.
“Bro hapo umezingua mm nmekuwa shabik yako tangu mwaka 2010 mpaka now nakubali kila ufanyacho bt kwahil nme kushusha vyeooo coz tambua ww ni mtot kisilam hapo ume feel bro nitaendelea kusapoti mziki wako ila tambua ume wakwaza wengi,” ameandika shabiki mmoja.
Baadaye alipost picha nyingine inayomuoesha hana kipino hicho kitendo kilichowafanya mashabiki wake wapumue. Lakini amekuja kuwatoa povu tena baada ya kupost video mbili zinazomuonesha akiwa amekirudisha kipini hicho.
“Bro sorry sana tunaokuelewa niwengi mno ila dah kwahiyo ishu unatupambanisha na maadui mana tunakosa majibu, kma kuna uwezekano m nahisi fanya utoe,” amemuomba shabiki mmoja kwenye video hiyo.
Seems like kipini cha pua bkwa mwanaume si kitu mtanzania anaweza kukielewa! Good news lakini ni kwamba reality TV show yake inakuja soon!
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment