Kama
za Kudumu za Kisekta leo zinatarajia kuanza kuchambua taarifa za
utekelezaji wa Bajeti za Wizara zinazosimamiwa na kamati hizo.
Hatua hiyo inafanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 98 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.
Akizungumza
jana Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge, Owen
Mwandumbya alisema kwa takribani siku tisa Kamati za Kisekta zitakuwa na
kazi ya kuchambua na kuangalia kama vipaumbele vimezingatiwa katika
bajeti ya wizara husika.
Mwandumbya
alisema katika kipindi hicho, Kamati ya Bajeti itafanya uchambuzi wa
Mapendekezo ya Mpango na kiwango cha ukomo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017.
“Kamati
zina mamlaka ya kuhamisha kasma moja kwenda nyingine, na kama inaona
kuna haja ya kupunguza au kuongeza bajeti ya wizara husika basi
mapendekezo hayo yanapelekwa kwenye Kamati ya Bajeti ambayo itashauriana
na Serikali,” alisema.
Mwandumbya
alisema kwa mujibu wa Kanuni ya 98(3) ya Kanuni za Bunge, Aprili 15,
mwaka huu kutakuwa na kikao cha pamoja kati ya Kamati ya Uongozi na
Kamati ya Bajeti ili kujadili mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati
za Kisekta wakati wa kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara
mbalimbali.
Juzi
Serikali iliwasilisha mbele ya wabunge wote Mapendekezo ya Kiwango na
Ukomo wa Bajeti kwa mwaka 2016/2017 inayotarajiwa kuwa ya Sh trilioni
29.539.
Post a Comment