RAIS
John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya
sherehe ya Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu Mei Mosi ambayo kitaifa
yatafanyika mkoani Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas
Mgaya alisema Tucta waliwasilisha maombi rasmi ya kumuomba Rais Magufuli
kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo na tayari wamepata taarifa
rasmi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Rais amekubali kuwa mgeni rasmi.
Mgaya
alisema hayo jana mjini Dodoma wakati wa mkutano baina ya Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma, Jordan Rugimbana na timu ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi
Kitaifa, ambao mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili na kuendelea
kuweka mipango na maandalizi ya kufanikisha sherehe za mwaka huu kwa
mafanikio makubwa.
Alisema
ili kufanikisha sherehe za Mei Mosi, Tucta Makao makuu watachangia nusu
ya gharama zote za sherehe nzima na nusu inayobaki itachangiwa na wadau
mbalimbali wakiwemo waajiri ambapo kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi
Bajeti nzima ya sherehe ya mwaka huu ni Sh milioni 29.6.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa Rugimbana aliishukuru Tucta na Serikali kwa
ujumla kwa kuupa Mkoa wa Dodoma ambao ni Makao Makuu ya Nchi heshima ya
kipekee ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya sherehe ya Sikukuu ya Mei
Mosi Kitaifa mwaka huu.
Naye
Katibu wa Tucta Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa alisema tayari
wameunda kamati ya maandalizi ya sherehe na jukumu kubwa lililoko mbele
ni kutafuta fedha na michango kutoka kwa wadau, wengi wao wakiwa ni
waajiri serikalini.
Post a Comment