Hatimaye uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam umekamilika leo katika ukumbi wa Karimjee, na kushuhudia Isaya Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Mwita ameibuka na ushindi na kutangazwa kuwa Meya Mpya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kupata kura 84 akimshinda mpinzani wake, Yenga Omary wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 67.
Uchaguzi
huo umeweka historia ambapo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa
mfumo wa vyama vingi (1992), Chama Cha Upinzani kimepata nafasi ya
kuongoza jiji hilo.
Uchaguzi
huo uliahirishwa mara kadhaa kutokana na mvutano uliokuwa unaibuka kati
ya wajumbe wa CCM na Chadema na kuzua vurugu wakati mwingine.
Tofauti
na ilivyo kwa tarehe nyingine za uchaguzi zilizopangwa na kuahirishwa
wakati wajumbe wakiwa ukumbini, viongozi wa ngazi za juu wa Chadema
pamoja na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward
Lowassa walihudhuria kushuhudia uchaguzi huo.
Post a Comment