Meneja wa Diamond, Babutale akishirikiana na Kalapina wamemchukua Chidi Benz na kumpeleka Life and Hope Rehabilitation Organization iliyopo Bagamoyo kwa ajili kumsaidiwa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
Hatua
hiyo imekuja baada ya hivi karibuni rapa huyo kuomba msaada baada ya
kuona ameshindwa kukabiliana na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa
yakimkabili.
Kupitia instagram, Babutale amepost video na kuandika:
"Mwana
amekubari kukaa Soba ila anasisitiza wana mje kumtembelea kumpa hope na
kuleta mapokopoko manjari. Mungu bariki hii safari ya matumaini"
Katika
video hiyo Babu Tale alisema wamefika salama Life and Hope
Rehabilitation Organization, Huku Kalapina akiomba mungu kumsaidia Chidi
Benz.
Post a Comment