Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni imebuni mbinu mpya
ya kushirikiana na wananchi kwa urahisi zaidi katika mapambano dhidi ya
rushwa kwa kusogeza huduma zake za kiofisi kwa kuwafuata wananchi na
kuweka ofisi katika eneo lililowazi ili Wananchi waweze kutoa kero zao
na kupatiwa ufumbuzi papo hapo.
Njia
hii ya ofisi inayotembea (mobile office) ilizinduliwa rasmi na Mkuu wa
TAKUKURU Mkoa wa kinondoni Bw. Benn Lincolin siku ya tarehe 23/03/2016
eneo la Bakhresa Manzese kwa kauli mbiu ‘Mwananchi ulipo TAKUKURU tupo
kutatua kero yako ya Rushwa kwa wakati’ inayoenda sambamba na kauli mbiu
ya Serikali ya awamu ya tano ya ‘ Hapa Kazi Tu’ kwa lengo la kutoa
huduma kwa kuwafuata wananchi mahali walipo na sio kwa kusubiri wao
kuleta malalamiko yao katika ofisi za TAKUKURU.
Imeonekana
kwamba njia hii itasaidia kutoa elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa
na kurahisisha ufuatiliaji wa fedha za miradi zinazotolewa kwenye
Manispaa. Pia itakuwa fursa nzuri ya kuwaelewesha wananchi kuhusiana na
sheria katika upatikanaji wa dhamana mahakamani na polisi.
Wito
unatolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo ofisi
hii inayotembea ya TAKUKURU Kinondoni itakapokua ili waweze kupata elimu
na kutatuliwa kero zao. Zawadi zitatolewa kwa mwananchi ambae atakua
akijibu vizuri maswali ya Chemsha Bongo kwani zoezi hili ni endelevu.
IMETOLEWA NA
MKUU WA TAKUKURU (M) KINONDONI
BENN LINCOLIN
30/03/2016.
Post a Comment