TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kumekuwa
na minongono mingi kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu Filamu ya
Mapenzi ya Mungu ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) iliyoshinda tuzo ya
Filamu bora Afrika Mashariki mapema mwezi huu huko Lagos Nchini Nigeria
katika tuzo za African Magic Views Choice Award (AMVCA).
Ili
filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa
kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo ambaye wazo hilo huwekwa katika
mswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa filamu.
Tunapenda
kuufahamisha umma kuwa mmiliki halali wa Filamu ya Mapenzi ya Mungu ni
Msanii Elizabeth Michael (Lulu) na ndiye aliyepata tuzo kwani ana haki
zote za kupata tuzo hiyo kama mmiliki halali wa filamu hiyo.
Filamu ya Mapenzi ya Mungu imetengenezwa chini ya kampuni ya Proin Promotion na imesajiliwa kwa namba ya usajili CO831190.
IMETOLEWA NA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
Post a Comment