Aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Edward Lowassa amewapa neno wanachama wa CCM wanaotaka
kufukuzwa ndani ya chama hicho wakituhumiwa kumuunga mkono.
Akiongea
hivi karibuni katika kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kilichofanyika
jijini Mwanza, Lowassa aliwasihi watu hao kujiondoa CCM na kujiunga na
Chadema kwani kuna maisha mazuri zaidi ndani ya chama hicho kikuu cha
upinzania.
“Lakini
hivi karibuni kuna utaratibu wa kuwafukuza kwenye chama watu ambao
waliniunga mkono. Wanafukuzwa wanaambiwa ‘ondokeni mfuateni Lowassa’.
"Nasikia
kuna mipango mikubwa zaidi baada ya mwezi wa sita atakapokabidhiwa Rais
Magufuli… kuna mipango mikubwa zaidi ya kuwaondoa kwenye chama,”
alisema Lowassa.
“Sasa
mimi nawaambia kwa niaba yetu. There is life outside CCM, nawaambia
tena kwa ajili yenu, waje Chadema kuna maisha mazuri tu hapa. Wasibaki
huko wananyanyaswa, wanabezwa wanafanya nini… waje tushirikiane tufanye
kazi,” aliongeza.
Lowassa
ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa CCM hivi sasa wanaumia kwa
sababu kuondoka kwake na kujiunga na Chadema kuliiongezea nguvu kambi
hiyo ya upinzani na kupunguza ruzuku kwa kiasi kikubwa kwa chama hicho
tawala.
Post a Comment