Kwa kutambua nafasi waliyonayo waandishi wa habari katika kuelimisha jamii kuhusu simu feki, Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imefanya semina na waandishi wa habari visiwani Zanzibar ili kuwapa uwezo wa kutambua simu feki ambazo kwa sasa zinaonekana kutumika kwa wingi nchini.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06# na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15 mfano IMEI 12456789067654 Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY C5555 – Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi
wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa
hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi
wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa
hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Waandishi
wakifuatilia mafunzo hayo kwa vitendo kuangalia somu zao kama ni
orijino baada ya kupata elimu hiyo ya kujua simu feki na orijino wakati
wa mkutano huo na Maofisa wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya
zanzibar ocean view kilimani zanzibar. kwa kuingiza namba waliopewa.
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA
Innocent Mungy, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari baada ya
kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba hizo na kugunduwa kuwa ziko
salama na siyo feki. kwa bahati nzuri takribani waandishi wote simu zao
orijino.
Post a Comment