Serikali
katika mwaka wa fedha 2015/2016 ilitenga Shillingi million 300 kwa ajili
matengenezo na ujenzi wa Barabara ya Kitosi- Wampembe katika Wilaya ya
Nkasi Mkoa wa Rukwa kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ili kufanya
Barabara hiyo iweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.
Akijibu
swali la Mhe. Desdelius John Mipata Mbunge wa Nkasi Kusini (CCM)
liliouliza ni lini Serikali itaitikia kilio hiki cha wananchi wanaopata
shida kwa Barabara hizo kutopitika katika kipindi chote cha mwaka,Naibu
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani
amesema Serikali kupitia Wizara yake imesikia kilio cha wananchi wa
Wilaya ya Nkasi na inaendelea kutoa fedha za matengenezo ya Barabara ya
Kitosi-wampembe.
“Kwa
mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitoa jumla ya Shillimgi Millioni 500
ili kufanya matengenezo ya Barabara ya Kitosi-Wampembe ili ziweze
kupitika katika kipindi chote cha mwaka,” alisema Mhe. Ngonyani.
Aidha
,katika kipindi cha mwaka wa fedha 2014/2015 Serikali ilitenga jumla ya
Shillingi Millioni 45 na Shillingi Millioni 60 zimetengwa katika mwaka
wa fedha 2015/2016 kwa ajili ya matengenezo ya aina mbalimbali ya
barabara ya Nkana-Kala kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili
kuhakikisha inapitika kwa kipindi chote cha mwaka.
Ukarabati
wa barabara ya Kitosi-Wampembe yenye urefu wa kilomita 67 na Barabara
ya Nkana –kala yenye urefu wa kilometa 68 uko chini ya Mfuko wa Barabara
ikisimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Barabara zote hizi ziko
chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambayo inawajibika kuwezesha
Barabara zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka.
Post a Comment