Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi imejipanga kudhibiti
uhalifu unaofanywa na na baadhi watu kwa kupora fedha za wafanyabiashara
au watu binafsi kwa kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama bodaboda.
Akijibu
swali la Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa Mbunge wa Biharamulo Magharibi
(CCM) lililouliza ni zipi takwimu sahihi za matukio ya ujambazi
yanayohusiana na uporajiwa fedha,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Mhe. Hamad Yussuf Massauni amesema matukio ya ujambazi yanayohusisha
uporaji wa fedha kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 kama
takwimu zinavyosema , kwa mwaka 2013 matukio 1.266, mwaka 2104 matukio
1,127 na mwaka 2015 yalikuwa 931.
”
Jeshi la polisi limechukua hatua kwa kufanya kazi karibu na mabenki
nchini ili kubaini kama kuna wafanyakazi wa mabenki wanashirikia na
majambazi kufanya uporaji huo na watakaobainika tutawachukulia hatua
kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani
watakaokamatwa”
“
Napenda kuwaomba wananchi kutupa ushirikiano na hasa kwa
wafanyabiashara wanaochukua fedha nyingi ili tuweze kuwapatia ulinzi ili
kupunguza, ama kuondoa kabisa vitendo hivi vya uporaji wa fedha
vilivyokothiri nchini kwa sasa” Alisema Mhe Massauni.
Aidha
amewaomba waheshimiwa Wabunge kutoa elimu kwa wananchi wao kuhusu
maswala ya ulinzi na usalama ili kupunguza vitendo vya uhalifu hasa
uporaji wa fedha kwa wafanyabiashara kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la
Polisi wakiona tukio lolote linalopangwa kwa ajili ya kupora fedha.
Serikali
kupitia Jeshi la Polisi linafanya ukaguzi wa pikipiki zote nchini ili
kubaini uhalali wake na uhalali wa wamiliki wake ili kuweza kubaini
pikipiki na wamiliki wanaohusika na vitendo vya uporaji wa fedha
vinavyoshamiri siku hadi siku
Post a Comment