Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Janeth Magufuli
ameziomba na kuzihamasisha taasisi za Serikali na zisizo za Serikali
kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili
Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu Wasiojiweza kijulikanacho kwa
jina la Nunge,viwemo vingine.
Aidha alisema vituo hivyo jumla vipo 17, katika maeneo mbalimbali nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mama Magufuli wakati alipotembelea makazi hayo
yaliyoko Kigamboni eneo la Vijibweni jijini Dares Salaam, ambapo
alisema changamoto wanazokabiliana nazo amezisikia na na aliwaahidi
kuwa atashirikiana na wadau wote kuzitafutia majibu yake.
Mama
Magufuli alizitaja baadhi ya changamoto hizo, kuwa ni uchakavu wa
miundombinu, uhaba wa rasilimali fedha na watu, pamoja na maslahi duni
ya watoa huduma, upungufu wa vitendea kazi na huduma za jamii, pamoja na
uvamizi wa eneo la kituo.
Aidha
Mama Magufuli alimwomba Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema
kulishughulikia taizo la uvamizi wa eneo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
“
Natumaini zawadi tuliyoileta ni ndogo na haiwezi kumaliza matatizo
yote mliyonayo. Lakini ni matumaini yangu kuwa zawadi hii inaweza kuwa
chachu ya kuhamasisha hamasa ya watu na vikundi vingine kujitoa kusaidia
watu wasiojiweza.
"Ni
imani yangu kuwa endapo watu wote tutajitoa kwa dhati tutaweza
kuwahudumia wazee na watu wasiojiweza na hivyo kuwapunguzia makali ya
maisha . Tukumbuke ‘kutoa ni moyo na si utajiri’ na kwamba “sisi sote ni
wazee na walemavu watarajiwa”.
Aliongeza
kwamba ni dhahiri kuwa Serikali ina wajibu mkubwa katika kuhudumia
wazee na watu wasiojiweza. Hata hivyo Serikali pekee haiwezi kumaliza
matatizo yote yanayowakabili na wazee na watu wasiojiweza.
Hivyo basi, sote kwa pamoja tunao wajibu wa kusaidia nguvu za Serikali katika kuwahudumia watu hao.
“Na
kwa kutambua hilo , mimi na wenzangu niliombatana nao tumeamua kutoa
zawadi yetu ndogo kwenu. Zawadi hiyo inajumuisha vitu vifuatavyo
mchele kilo 3000, unga kilo 3000 na maharage kilo 1200. Kulingana na
idadi yenu niliyopewa kila mmoja atapewa kilo 25 za mchele, kilo 25 za
unga na kilo 10 za maharage.
“Nawaombeni
mniruhusu pia kuchukua nafasi hii kuwasilisha kwenu salamu nyingi
kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
"Ameniomba
niwaarifu kuwa yupo pamoja nayi na kwamba Serikali itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu
wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu kwa kadri ya uwezo wake,” alisisitiza Mama Magufuli.
Mama Magufuli aliongeza kwamba wazee na watu wasiojiweza wanahitaji upendo, kuthaminiwa nakusaidiwa.
Hivyo
kipimo kimojawapo cha kupima jamii iliyostaarabika na inayoheshimu
misingi ya utu ni kuangalia namna inavyo wathamini wazee na watu
wasiojiweza.
Aliupongeza
uongozi na watumishi wote wa kituo hicho na vituo vingine nchini kwa
kazi kubwa wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke , Sophia Mjema alimtaka kila
mwananchi kutambua kwamba bila wazee hakuna tutakachoweza kufanya hivyo
ni muhimu kuwa enzi na kuwasaidia wazee walioko majumbani na mitaani.
“Tuwaenzi
wazee na kuwasaidia pia hata wale walioko mitaani tuwashauri warudi
majumbani ili Serikali iweze kuwaorozesha kwa kuwa si vizuri kukaa
barabarani, Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli itahakikisha
inawajali wazee,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu watoto wa mitaani alisemani wajibu wa wazazi kuhakikisha
wanawalea watoto wao vizuri ili wasikilimbile mitaani kwa kuwa watoto ni
taifa la kesho.
Naye
Mwenyekiti wa wazee wa makazi hayo, Anthony Kikongoti alimshukuru Mama
Magufuli kwa niaba ya wenzake, kwa kuanza ziara yake ya kwanza ya
kutembelea kituo hicho ,ambapo alimwomba apeleke salamu zao kwa baba
yao ambaye ni Rais Magufuli kuwa wanasema asante.
“Huu ni mwaka wa wanyonge dini zote tumwombee kwa pamoja ili aweze kuendelea kupunguza makali ya maisha,” alisema.
Afisa
Mfawidhi wa kituo hicho, Ojuku Mgedzi alisema wanahitaji bajeti ya
kutosha ya kuendesha shughuli mbalimbali, watumishi 42 , wakiwemo
walinzi, kwa kuwa waliopo sasa ni 29 na hawatoshi.
Alisema eneo hilo lina hekari 50.8 na nusu ya eneo hilo limevamiwa.
Mgedzi alisema kituo hicho kina idadi yawakazi 112, ambapo alimkabidhi Mama Magufuli orodha ya idadi ya watu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku
Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Bw. Ojuku
Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akioneshwa maeneo mbalimbali na Bw. Ojuku
Mgedzi, Mkuu wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wagonjwa waliofika kupata
huduma katika zahanati ya Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu
cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza
mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000
na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akitembelea chumba cha kujifungulia cha
zahanati ya Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge,
Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao
pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage
Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana kwa furaha na wakaazi wa
Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini
Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa
msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa
msaada wake kwa wazee na walemavu hao.
Mkuu
wa wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema akimkaribisha Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli kuhutubia wakaazi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu
Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam alikotembelea na
kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga
kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu
hao.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wakaazi wa Kituo cha Makazi ya
Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigambo ni, jijini Dar es salaam
alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa
mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake
kwa wazee na walemavu hao.
Post a Comment