Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko,,
amemtaka waziri mkuu wa nchi hiyo kuachilia madaraka, kwa maelezo kwamba
amepoteza imani na uungwaji mkono na umma wa nchi hiyo ikiwemo serikali
ya muungano.
Kauli ya rais Poroshenko ilikuja muda mfupi kabla waziri mkuu, Arseniy Yatsenyuk, hajalihitubia bunge la nchi hiyo mjini Kiev.Bwana Yatsenyuk aliwaambia wabunge kwamba baraza lake la mawaziri limejitahidi kutimiza wajibu wake katika wakati mgumu , na kusema kwamba alikuwa akitarajia kupata upinzani mkali na kura ya hapana katika utendaji wake.
Waziri mkuu huyo ameingia lawamani kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya kukithiri kwa rushwa nchini humo.Na katika siku za hivi karibuni lilipitishwa azimio la kumtaka waziri huyo aachilie madaraka kwa kutowajibika ,na hatua hiyo iliibua maswali yasiyokuwa na majibu katika serikali za ukanda wa umoja wa ulaya na hata shirika la fedha ulimwenguni IFM.
Post a Comment