Friday, 12 February 2016
Waziri Nchemba Afanya Ziara Ya Kushtukiza Saa Saba Usiku Machinjio Ya Ukonga Mazizi Na Kufukuza Viongozi Wote Wa Machinjio
Posted by Unknown on 07:37:00 in | Comments : 0
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usiku wa kuamikia leo katika Machinjio ya Ukonga Mazizi.
Katika ziara hiyo, Waziri Nchemba amekamata ng'ombe 200 wakiwa wanaingizwa kwenye machinjio bila kibali halali, na kati yao ni ng'ombe 20 tu ndo walikuwa na kibali cha kuchinjwa, hivyo ushuru wa ng'ombe 180 ulikuwa unatafunwa na watumishi waovu.
Baada ya kubaini hali hiyo,Waziri Nchemba ameufukuza uongozi wote wa machinjio hayo na kuagiza vyombo vya dola viwakamate viongozi wote waliohusika na kuwafikisha mahakamani.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment