Thursday, 11 February 2016
Papa yuko tayari kuianza ziara ya Kitume ya 12 nchini Mexico
Posted by Unknown on 21:03:00 in | Comments : 0
Baba Mtakatifu Francisko, akiijipanga sawa kuianza safari ya Kitume ya kimataifa ya 12 nchini Mexico, Alhamisi hii kabla ya adhuhuri, alikwenda kimyakimya katika Kanisa Kuu la Maria Mkuu la hapa Roma, kutolea sala zake, kama afanyavyo siku zote kabla ya kuaza safari za kimataifa, kuomba Mama Bikira Maria wa Salus Popoli Romano, anayeheshimu sana na wakazi za jiji la Roma, aandamane nae ziarani. Baada ya hapo Papa alikwenda katika Kanisa Kuu la Yohane wa Lateran, ambako alikutana na Mapadre wa Jimbo la Roma , kama ishara ya kuzindua rasmi mwanzo wa kipindi cha Kwaresima, ambako pia aliwaungamisha Mapadre kadhaa.
Kardinali Augostino Vallini, Vika wa Jimbo la Roma, akirejea tukio hili la Mkutano wa Papa na Mapadre wa Jimbo la Roma, majadiliano yake zaidi yalilena katika kipindi cha hiki cha mafungo ya Kwaresima na yaliyomo katika barua iliyokwisha chapishwa katika tovuti ya Vikariati ya jimbo la Roma, juu ya Mapadre kuonyesha Huruma ya Mungu katika kazi za jamii waliokabidhiwa . Mkutano huo uliongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo la Roma, Angelo De Donatis, ambaye ni Mwenyekiti Kitengo cha Huduma kwa Mapadre katika Jimbo la Roma .
Kama ishara ya huruma katika kipindi cha Kwaresima, mchango wa fedha wa Mapadre, uliokusanywa katika tukio hili, unapelekwa kitengo cha Caritas cha Jimbo la Roma.
Na mwisho Kardinali Vallini alitangaza kwamba, Papa ametoa zawadi ya kitabu chake kinachoitwa 'Jina la Mungu ni Huruma" , kwa Mapadre wote wa Jimbo la Roma.
Mungu ni Huruma , kwa makuhani na viongozi wote wa dini wa Jimbo la Roma. ya Kirumi.
Ziara Mexico
Baba Mtakatifu Francisco,Ijumaa ya wiki hii, majira ya saa mbili za usiku, anakwenda Mexico ambako atakuwa na ziara ya kitume , kwa muda wa siku sita tangu 12-17 Februari, akifuata nyayo za watangulizi wake Papa Yohane Paulo 11 na Papa Bnedikto XVI, kwenda kukutana na wanakondoo wake wanaomsubiri kwa hamu , kama baba anayerejea nyumbani, akiwa na kifurushi cha chakula kwa watoto wake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment