Monday, 22 February 2016
Papa awataka wafanyakazi wa Curia na Vatican kuwa watu wa huruma
Posted by Unknown on 23:07:00 in | Comments : 0
Mkiwa Wafanyakazi wa Vatican na Ofisi za Jimbo Takatifu , ni lazima kila siku kuruhusu huruma ya Mungu itende kazi ndani ya mioyo yenu, na katika kuwa mashahidi wa manufaa ya kukiri imani kwa Kristo. Ni Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Jumatatu hii, wakati akiongoza Ibada ya Misa kwa ajili ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilee ya Huruma ya Mungu kwa Wafanyakazi wa Idara za Curia ya Roma , na Taasisi zote za Vatican. Kabla ya Ibada , wafanyakazi hao waliandamana na Baba Mtakatifu tokea Ukumbi wa Paulo VI na kupita katika Mlango Mtakatifu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kukusanyika katika Madhabahu ya Kuu ya Kaburi la Mtume Petro kwa ajili ya kikukiri imani yao . Papa kwa namna ya kipee aliombea utendaji wao, uangaziwe na Neno la Mungu, wakifuata mfano wa Mchungaji Mwema , katika kuliongoza Kundi la Kristo, yaani Kanisa. .
Homilia ya Papa alilenga katika uthabiti wa kuikiri imani , akitazamisha katika swali la Yesu "Na ninyi je, mwasema mimi ni nani? (Mt 16:15)”. Swali alilolitaja kuwa ni swali wazi na la moja kwa moja, ambalo si rahisi kulikwepa nahalina ugumu katika kutoa jibu. Na hivyo alimtaka kila mmoja, ndani ya moyo wake, kutoa jibu kwa uaminifu. Alisema Yesu hakuuliza swali hili kw ania za udadisi tu, lakini kama swali msingi lenye kuonyesha upendo kamili wa Yesu! Ni swali linalomtaka Mkristo kuonyesha hali y aimani yake kwa Kristo. Imani yenye kuonyesha kumtambua kuwa Kristo kuwa ndiye Mwana wa Mungu na Bwana wa maisha. Papa amesemani wito mpya na wa kwanza katika kuikiri imani, na hasa kwa kazi za mwandamizi wa Petro, ambaye hawezi tangamana na jukumu la kuwaimarisha nduguzake katika Kristo Lk 22:32).
Baba Mtakatifu Francisko aliendelea kuwataka wafanyakazi wa Vatican na idara zake , kuachia neema za Mungu , kuunda upya mioyo yao katika imani na kufungua midomo yao na kudumu katika kuiugama imani na wokovu waliopokea(Rum 10:10). Na hivyo wote wanapaswa kujibu kama Mtume Petro : "Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai" (Mt 16:16). Kwa hiyo mawazo yao na macho yao na utendaji wao wote , vinatakiwa kuitazama sana sura ya Yesu Kristo, aliye mwanzo na mwisho wa kila shughuli ya Kanisa. Yeye ni jiwe la msingi la kazi zote za Kanisa na hakuna mtu anayeweza tengua ukweli huo na maelezo tofauti (1 Wakorintho 3:11). Kristo ndiye "mwamba" ambayo ni lazima kazi zote za Kanisa kujenga juu yake.
Aidha Papa alikumbusha maana ya maneno ya Mtakatifu Augustine anapoandika juu ya misukosuko, machafuko na matukio ya kihistoria akisema kwamba havikulizima Kanisa, kwa kusababu Kanisa limejengwa juu ya mwamba ambao Petro aliitwa kw ajina hilo. Ni mwamba ambao Petro alipata uimara wake na si mwamba ulichota uimara wake toka kwa Petro,. Na ndivyo kwa namna hiyo hiyo, kwamba Kristo jina lake halitokani na Mkristo lakini Mkristo hupata jina lake kutoka kwa Kristo. Mwamba ni Kristo, msingi wa ambao juu yake Petro, analijenga Kanisa la Kristo(Yn 124, 5: PL 35, 1972).
Baba Mtakatifu aliendelea kuzungumzia haja ya kila mmoja kukiri imani yake kwa uthabiti, kama wajibu kwa kila aliyeitwa katika huduma za Kanisa, na hasa kwa Wachungaji, juu ya yote, wanatakiwa kuishi kama mfano wa Mungu mwenyewer ambaye huliongoza kundi lake, kama Nabii Ezekieli alivyoutaja utendaji wa Mungu kwamba: Yeye huenda katika kutafuta kondoo waliopotea,huwageukia wale walioumizwa au kujeruhiwa kiroho kuwatibu magonjwa yao Hiyo ndiyo tabia anayotakiwa kuwa nayo mchungaji , kuwa na huruma isiyokuwa na mipaka. Kuwa mchungaji ni majitoleo katika kina cha imani tena mara kwa mara, bila masharti, kwa sababu wote ni dhaifu wenye kuhitaji kuifikia huruma ya Mungu.Alieleza kwa kurejea tena utabiri wa Nabii Ezekieli , kwa viongozi wa wana wa Israel,ambamo aliwataka viongozi hao kwanza waanze kujichunguza mapungufu yao wenyewe. Na ndivyo ilivyo kwa , aliyeitwa kuwa Mchungaji katika Kanisa, kwanza aruhusu kuangaziwa na uso wa Mungu Mchungaji Mwema, kuruhusu kusafisha nae na ubadilisha maisha kwa kufanya ukarabati kamilifu wa dhamira, ili kwamba hata katika mazingira ya kazi, waweza kusikia kwa nguvu, wito wao wa kuwa wachugaji , hasa kwa watu wanaokutana nao siku hadi siku, ili kwamba kusiwe na mtu anayejisikia kupuuzwa au kutendewa vibaya, lakini kila mtu aweze kuishi kwa furaha ya kuwa karibu na mlezi wenye upendo wa Mchungaji Mwema.
Papa amewaambia kwamba, wao daima wameitwa kuwa washirika wa Mungu katika kufanikisha kazi yake muhimu na ya kipekee ya kuwa shahidi wa nguvu wa neema ya Mungu yenye kubadilisha maisha kwa nguvu za Roho anayeleta upya.
Baba Mtakatifu alieleza na kumtaka kila mmoja amwachie Bwana amwokoe dhidi ya kila jaribu, linalotaka kumweka mbali na dhamiraza kumtumikia Bwana, na katika kugundua upya uzuri wa kuikiri imani kwa Bwana Yesu Kristo. Aliongeza uaminifu katika utendaji wa kazi huenda sambamba na huruma ya Mungu, tunayotakiwa kuiishi kila siku. Na kwamba katika Maandiko Matakatifu, kwa hakika, uaminifu na huruma haviwezi kutenganishwa, ni mambo yaliyoshikamana pamoja. Mahali palipo na uaminifu pia kuna huruma, ni mambo yaliyoungana yanayo onyesha uwepo wa sura ya Mchungaji Mwema. Alikumbusha, uaminifu unahitaji kutenda kwa mujibu wa moyo wa Kristo. Kama Mtume Petro alivyosema , ni lazima kulisha kundi kwa roho ya ukarimu" na kuwa "mfano" kwa wote, ili wakati Mchungaji Mkuu Mwema atakarudi, wawe na uwezo wa kupokea "taji ya utukufu isiyonyauka “ (1Pet 5:14).
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment