BREAKING NEWS

Monday, 22 February 2016

Obasanjo: Uganda haipaswi kuzuia upinzani




Aliyekuwa rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ametaka pande zote pinzani katika uchaguzi wa Uganda kujiepusha na matamshi ya uhasama.
Obasanjo ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya madola uliokuwa ukiangalia vigezo vya kidemokrasia katika uchaguzi uliokamilika nchini Uganda amewashauri viongozi wa uganda kujiepusha na makabiliano na migongano baina yao.
Obasanjo alisema''Uhuru wa kujieleza kutengamana na kuwasilana na umma wa kila kiongozi sharti ulindwe na kama kuna vizuizi dhidi ya kiongozi yeyote lazima iondolewe mara moja''




Obasanjo aliyasema hayo bila ya kumtaja kiongozi wa upinzani Kizza Bisigye ambaye kwa sasa amezuiliwa nyumbani kwake.
Aliongezea kuwa ''dosari zilizoshuhudiwa katika uchanguzi mkuu umekuwa na madhara mabaya kwa matokeo ya ukweli haki na uwazi wa uchaguzi huo'' , lakini amesisitiza tofauti kati ya utawala na upinzani zinahitajika kusuluhiswa kupitia mazugumzo.''
Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda alikamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.



Amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo.
Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake.
Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree