BREAKING NEWS

Monday, 22 February 2016

Mkuu wa riadha Kenya apigwa marufuku miezi 6





Shirikisho la riadha duniani IAAF, limempiga marufuku mkurugenzi mkuu wa shirikisho la riadha la Kenya bwana Isaac Mwangi kwa siku 180.
Bwana Mwangi anatuhumiwa kwa kuwaitisha hongo wanariadha wawili waliopatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini ilikupunguza kipindi cha marufuku yao.
Mwangi amekanusha madai dhidi yake.
Mkurugenzi huyo mkuu tayari alimejiondoa kwa siku 21 ilikufanikisha uchunguzi dhidi yake.
Kufuatia marufuku hii yakamati ya maadili basi bwana Mwangi hatakuwa na mchango wowote katika mashindano ya olimpiki yatakayofanyika mjini Rio Brazil mwaka huu.
Kupitia kwa taarifa maalum mkuu wa kamati ya maadili bwana Michael Beloff QC amepigwa marufuku kwa kujaribu kuhujumu kampeini dhidi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini.
Marufuku yake inaanza mara moja yaani kuanzia tarehe 22 mwezi Februari 2016.


Uchunguzi huu hautaathiri kwa vyovyote vile uchunguzi unaoendeshwa na mchunguzi mkuu wa kamati ya maadili ya IAAF jaji Sharad Rao.
Mkurugenzi huyo alijipata matatani baada ya wanariadha wawili Joy Sakari na Francisca Koki Manunga kudai kuwa Mwangi alikuwa amewaitisha hongo ya takriban dola elfu hamsini ilikupunguza kipindi cha marufuku.
Wawili hao walipatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini katika mashindano ya riadha duniani yaliyofanyika huko Beijing Uchina.
Habari hizi zinatokea juma moja tu baada ya rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF Lord Sebastian Coe kutishia kuipiga marufuku Kenya kutoshiriki michezo ya Olimpiki yanayoratibiwa kufanyika mwezi Agosti.




Wanariadha 40 wa Kenya wamepatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu mwilini katika kipindi cha miaka 3 iliyopita.
Kenya inatarajiwa kuorodheshwa miongoni mwa mataifa yanayomulikwa kwa kushindwa kuafikia mahitaji hayo ya WADA na huenda ikapigwa marufuku kushiriki katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa na wanariadha wa Urusi.


Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree