Kampuni ya kutengeneza simu ya Samsung imezindua simu yake mpya ya kisasa aina ya Galaxy S7 na Galaxy S7 Edge.
Kampuni
hiyo ya kutokea Korea Kusini imezindua simu hizo mbili ilikukabiliana
na upinzani mkali kutoka kwa kampuni ya simu ya Apple.Simu hizo za Galaxy S7 zimerejeshewa uwezo wa kusoma kadi ya kuhifadhia data al maarufu (MicroSD card)
Kikubwa kitenolojia katika simu hizo mpya za Galaxy S7 ni kuwa zinaweza kutumika hata ndani ya maji bila ya kuharibika.
Vile vile Galaxy S7 zina programmu iliyoimarishwa zaidi mbali na kuwa na kamera ya nyuma yenye uwezo wa kupiga picha hata kwenye mazingira yenye giza totoro na picha hizo zikaonekana bora.
Wadadisi wa maswala ya teknolojia hata hivyo hawaoni tofauti kubwa kimsingi kati ya simu hiyo ya Galaxy S7 na ile ya awali ya Galaxy S6 .
Hilo ndilo litakalowasumbua wauzaji wa simu hiyo mpya kwani umbo na ukubwa wake ni sawasawa na ile ya Galaxy S6.
''Tunafurahia kuwa sasa tunaweza kuimarisha uwezo wake mkubwa wa kuhifadhi data kupitia kadi hiyo ya (MicroSD card) pia unaweza kupiga picha hata kwenye mazingira ya giza mbali na kuwa hata ukinyeshewa unahakika kuwa simu yako haitazima lakini kwa umbo ,,,la hapo wameboronga bwana ! alisema Ian Fogg kutoka kampuni ya kutathmini teknolojia IHS Technology.
''Ninashindwa kwa hakika kuelezea mtu tofauti kati ya simu hii ya Galaxy S7 naile ya Galaxy S6''
Samsung huwa haitangazi idadio ya simu ilizouza.
Hata hivyo idadi ya mauzo ya kampuni hiyo ilizorota kwa asilimia 2% katika mwaka wa 2015.
Wapinzani wake wakuu Apple, Huawei na Xiaomi hata hivyo walisajili kuimarika kwa faida zaidi.
Takwimu ya kampuni moja ya mauzo ya teknolojia IDC inaonesha kuwa kampuni hiyo ya Korea Kusini ni bora zaidi katika mauzo ya simu katika vitengo tofauti kote duniani.
Simu hiyo mpya ya Galaxy S7 inaurefu wa nchi 5.5in (14cm).
Simu ya awali ya Galaxy S6 inaurefu wa nchi 5.1 (13cm)
Post a Comment