Mshambuliaji amefyatua risasi katika
ofisi ya idara moja ya elimu nchini Saudia, kusini mwa mkoa wa Jazan,na
kuwauwa wafanyikazi wengine sita ,maafisa wamesema.
Watu wengine
wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo,lililofanyika katika jamii ya
mashambani ya Ad Dair,karibu na mpaka na Yemen.Mshambuliaji huyo amekamatwa ,afisa mmoja amesema.
Hakuna sababu ya shambulio hilo iliotolewa,na mamlaka inasema kuwa inalichukulia swala hilo kama la uhalifu.
Mshukiwa huyo hajajulikana lakini, kituo cha habari cha AFP,kikinukuu runinga ya Al-Ekhbariya ,imeripoti kwamba mtu huyo hakuwa mfanyikazi lakini alikuwa na biashara katika wizara hiyo.
Ripoti za awali zilsema kuwa mshambuliaji huyo alikuwa mwalimu.
Post a Comment