Kampuni kubwa ya chakula pamoja na
vinywaji Nestle imevunja ufadhili wake katika shirika la riadha duniani
IAAF ,ikihofia kwamba kashfa ya utumizi wa dawa za kusisimua misuli
inyokumba shirika hilo huenda ikaharibu sifa zake.
Kampuni hiyo kutoka Uswizi imesema kuwa imechukua uamuzi huo mara moja.Hatahivyo ,rais wa shirikisho hilo Lord Coe amesema kuwa amekasirishwa na uamuzi huo na hataukubali.
Mwezi uliopita,kampuni ya nguo za michezo Adidas ilivunja mkataba wake na shirikisho hilo.
Tumeamua kuvunja uhusiano wetu na mpango wa riadha miongoni mwa jina katika IAAF mara moja.
Uamuzi huu unatokana sifa mbaya kutoka kwa umma kutokana na madai ya ufisadi na utumizi wa dawa za kutumia nguvu dhidi ya IAAF.
Tunaamini kwamba hili huenda likaathiri vibaya sifa na sura yetu na hivyobasi tumevunja mkataba wetu na IAAF,ulioanzishwa 2012.
Tumeelezea IAAF kuhusu uamuzi wetu na sasa tunasubiri jibu lao kwamba ushirikiano wetu umekwisha.
Post a Comment