BREAKING NEWS

Wednesday, 24 February 2016

Acheni kuharibu vyanzo vya maji

WITO umetolewa kwa jamii kuacha tabia  ya kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji ama maeneo kuzunguka Milima ya Uluguru ili kuepusha  na uharibifu wa mazingira.


Wito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Shirika  linalojihusisha na uhifadhi  wa mazingira  na uhamasishaji Mkoani Morogoro ‘’Tanzania environmental and suntation  concervetors (TESCO) Ndumey Mukama wakati akizungumza na Mtanzania ofisini kwake.

Mukama amesema  kuwa  uharibifu wa mazingira umekuwa ukifanyika katika vyanzo vya maji na maeneo yanayozunguka milima ya Uluguru na hiyo inatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa utuzaji wa mazingira.

Aklitolea mfano  wananchi wamekuwa wakivuka mipaka ya milima  ya Uluguru  na kufanya shughuli za kibinadamu na hivyo kuharibu uoto wa asili.

Amesema  kuwa bado  kuna changamoto ya utiririshaji wa maji machafu  katika mabomba na pia katika mito ambayo wananchi wanatumia maji hayo katika shughuli mbalimbali.

.
Aidha amesema  kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo za uharibifu wa mazingira Shirika limekuwa likitoa elimu ya mazingira mara kwa mara ili kuwajengea wananchi uelewana kuona umuhimu wa utunzani  mazingira yanayowazunguka.

Hata hivyo amesema  kuwa wamejaribu  kutoa elimu ya mazingira ili wananchi waache tabia ya kuchoma mioto katika safu za milima ya Uluguru  lakini bado vitendo hivyo vya uharibifu wa mazingira vinaendelea.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree