BREAKING NEWS

Wednesday, 24 February 2016

TAARIFA YA HABARI ZA KANISA



JUMATANO  24/2/2016………………………………………..
========================================
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashari na Kati, AMECEA kwa kushirikiana na Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kikanda, Caritas, wameamua kwa pamoja kulivalia njuga tatizo la ukosefu wa usawa pamoja na umaskini unaowakabili wananchi wengi wa Afrika Mashariki na Kati.
========================================
PADRE Gaitan Mwaswenya Paroko wa Parokia ya mtakatifu Gaspali Makole amewataka Wakristu katika kipindi hiki cha Kwaresma wasikchukulie kuwa ni cha mazoea bali wakitumie vizuri kwa kunyoosha mapito na kufikia mabonde pamoja na kuraluwa nyoyo zao.

                                          NA
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya hivi karibuni limeadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Kenya kuanzia tarehe 25- 27 Novemba 2015.
HABARI KAMILI,
    


KWA KUMALIZA TAARIFA YA HABARI SIKILIZA TENA MUHTASARI WAKE  
JUMATANO  24/2/2016………………………………………..
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashari na Kati, AMECEA kwa kushirikiana na Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kikanda, Caritas, wameamua kwa pamoja kulivalia njuga tatizo la ukosefu wa usawa pamoja na umaskini unaowakabili wananchi wengi wa Afrika Mashariki na Kati.
========================================
PADRE Gaitan Mwaswenya Paroko wa Parokia ya mtakatifu Gaspali Makole amewataka Wakristu katika kipindi hiki cha Kwaresma wasikchukulie kuwa ni cha mazoea bali wakitumie vizuri kwa kunyoosha mapito na kufikia mabonde pamoja na kuraluwa nyoyo zao.

                                          NA
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya hivi karibuni limeadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Kenya kuanzia tarehe 25- 27 Novemba 2015.

NA HUO NDIO MWISHO WA HABARI ZA KANISA




NAIROBI                    SAA 10.00JIONI                    24.2.2016
Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashari na Kati, AMECEA kwa kushirikiana na Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kikanda, Caritas, wameamua kwa pamoja kulivalia njuga tatizo la ukosefu wa usawa pamoja na umaskini unaowakabili wananchi wengi wa Afrika Mashariki na Kati.
Maamuzi haya yamefikiwa kati ya AMECEA na Wakurugenzi wa Caritas kutoka katika Mabaraza ya Maaskofu Katoliki yanayounda AMECEA, katika mkutano wake uliofanyika hivi karibuni Jijini, Nairobi, Kenya.
AMECEA na Caritas wanasema, wameamua kutekeleza changamoto inayotolewa na Baba Mtakatifu Francisko katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro kwa kutoa kipaumbele cha pekee katika kupambana na umaskini, kwa kushikamana na maskini na kwa ajili ya maskini, kama njia ya kutoa huduma makini kwa Familia ya Mungu.
Huduma hii inakwenda sanjari na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote, huduma za kijamii pamoja na amani huduma ambazo zinapaswa kububujika kutoka katika undani wa mtu.
AMECEA na Caritas wameamua kushirikiana kwa dhati katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, kwa kubadilishana taarifa, ujuzi na mang’amuzi, ili kweli familia ya Mungu Afrika Mashariki iweze kushiriki kikamilifu katika mapambano ya biashara hii inayodhalilisha utu na heshima ya binadamu.
Biashara hii kwa upande mwingine inafumbatwa pia katika wimbi kubwa la wahamiaji na wakimbizi, Wanapenda kushughulikia haki, amani na maridhiano; kwani ukosefu wa tunu hizi msingi katika nchi nyingi za AMECEA kumepelekea makundi makubwa ya wahamiaji.
RV/SL                                        MWISHO.

ROMA                           SAA 10.00JIONI                           24.2.2016
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio yenye makao yake makuu mjini Roma inaunga mkono juhudi za Baba Mtakatifu Francisko za kutaka Jumuiya ya Kimataifa kufuta adhabu ya kifo kwani imepitwa na wakati.
Maoni ya wengi yanaonesha kwamba kuna uwezekano wa kudhibiti uhalifu bila kusababisha mauaji ya wahalifu.
Maisha ya binadamu ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo inapaswa kuendelezwa na kudumishwa.
Baba Mtakatifu anawasihi viongozi Wakatoliki wakati huu wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu kutoridhia utekelezaji wa adhabu ya kifo katika nchi zao.
Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Jumatatu tarehe 22 Februari 2016 imeendesha kongamano la kimataifa dhidi ya adhabu ya kifo duniani kwa kuwashirikisha mawaziri wa sheria kutoka katika nchi 30 ili kuridhia mchakato wa kufuta adhabu ya kifo duniani.
 Kumekuwepo na maendeleo makubwa tangu mwaka 2014, Baraza kuu la Umoja wa Mataifa liliporidhia ufutaji wa adhabu ya kifo.
Mongolia na Pwani ya Pembe ni kati ya nchi ambazo zimefuta adhabu ya kifo kutoka katika Sheria za nchi.
Wachunguzi wa mambo wanasema mahali ambapo kuna vitendo vya kigaidi, maoni ya wengi ni kuendeleza adhabu ya kifo!
Takwimu zinaonesha kwamba, kuna nchi 105 ambazo zimekwishafuta adhabu ya kifo na nyingine 43 kwa miaka mingi hazijawahi kutekeleza adhabu ya kifo, ingawa imeandikwa kwenye Katiba na Sheria za nchi husika,hata hivyo adhabu ya kifo katika kipindi cha miaka miwili imetekelezwa katika nchi 22 duniani.
RV/SL                                                   MWISHO.
DODOMA                   SAA 10.00JIONI                 24.2.2014
PADRE Gaitan Mwaswenya Paroko wa Parokia ya mtakatifu Gaspali Makole amewataka Wakristu katika kipindi hiki cha Kwaresma wasikchukulie kuwa ni cha mazoea bali wakitumie vizuri kwa kunyoosha mapito na kufikia mabonde pamoja na kuraluwa nyoyo zao.

Amesema kuwa Kwaresma ni kipindi kitakatifu cha kujirudi kujisafisha,amesema kuwa hatari ambayo anaiona sasa ni kuhangaikia vyakula na mavazi mambo ambayo hayana tija katika maandiko matakatifu.

Padre Mwaswenya amesema kuwa kipindi cha mfungo wa Kwaresma kinawataka Waamini kuacha uchafu wote ikiwa ni pamoja na wizi,chuki,unyanyasaji,usengenyaji na mambo yote mabaya.

Akizungumzia kipindi cha jubilee ya huruma ya mungu ambacho kimetangazwa na Baba mtakatifu Francis,Padre Mwaswenya ameeleza kuwa ni wakati muafaka kwa wakatoliki kumuomba mungu huruma yake ili aweze kuwasaidia,wagonjwa,wenye shida na wanaoteseka kutokana na kadhia mbalimbali.

Amesema kuwa Jubilei ya mwaka wa Huruma ya mungu pia inatutaka sisi waamini kuwa na huruma kwa wengine kama ambavyo mama Kanisa alivyokuwa na huruma kwetu sisi.

NGOI/SL                                                    MWISHO.
NAIROBI                   SAA 10.00JIONI                   24.2.2016
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya hivi karibuni limeadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kufanikisha hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Kenya kuanzia tarehe 25- 27 Novemba 2015.
Ibada hii imeongozwa na Kardinali John Njue, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Nairobi na kuhudhuriwa na Maaskofu, Wakleri, Watawa na Waamini walei pamoja na wawakilishi wa viongozi wa Serikali nchini Kenya.
Askofu Peter Kihara wa Jimbo Katoliki la Marsabit, Kenya katika mahubiri yake amesema kwamba, hija ya Baba Mtakatifu nchini Kenya imekuwa ni kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Familia yote ya Mungu nchini Kenya.
Watu wengi wamevutwa na kuguswa na mahubiri pamoja na hotuba za Baba Mtakatifu Francisko zilizogusa kwa undani matatizo, changamoto na matumaini ya familia ya Mungu nchini Kenya.
 Baba Mtakatifu katika hija yake ya kitume nchini Kenya, aliwataka wakenya kujikita katika mchakato wa majadiliano ya kidini na kiekumene kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wengi.
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya linamshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kuweza kufuata na kutekeleza ratiba ngumu iliyokuwa mbele yake wakati wa hija yake ya kitume nchini Kenya, licha ya umri wake, Wanamshukuru kwa kuamua kutembelea Kenya ili kuwaimarisha ndugu zake katika imani, matumaini na mapendo. Mahubiri na ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko nchini Kenya kwa sasa umewekwa kwenye vitabu na DVD tayari kuwasaidia wananchi kufanya rejea kwa tukio hili la kihistoria nchini Kenya.
RV/SL                                                   MWISHO.

DODOMA                     SAA 10.00JIONI               24.2..2.2016
IMEELEZWA kwamba Wakristu ambao hawatoi fungu la kumi wanamwibia mungu hivyo wameaswa kujitambua na kutoa sadaka na kusaidia wengine wenye uhitaji kama vile yatima,wajane,masikini na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa huduma ya Injili na umisioni wa Kanisa la FPCT Jimbo la Dodoma,mchungaji Erasto Hussein wakati akitoa neno la mungu kwenye Ibada ya kuchangia mfuko wa huduma hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Kanisa la FPCT Chan”gombe mjini Dodoma.

Mchungaji Hussein ambaye pia anahudumia Parish ya Ihumwa amesema kuwa lengo la mfuko huo ni kutangza Injili kwa watu wasiofikiwa,ujenzi wa majengo ya Makanisa ya kisasa na kuondokana na Makanisa ya tembe.

Aidha mchungaji huyo ametoa wito kwamba Makanisa yasiwe vijiwe vya kujifichia,mafisadi,wala rushwa,majambazi,wauza dawa za kulevya na waharifu wengine.

Mchungaji Hussein pia ameshangazwa kuona baadhi ya wachungaji ambao wamekuwa na mfumo wa kuhubiri Injili kwa njia ya ukali na kufoka kwa waamini wao ,hali hiyo husababisha makanisa yao kukimbiwa na waamini
NGOI/SL                                                         MWISHO.

MPWAPWA                    SAA 10.00JIONI                  24.2.2016

Waumi wa kanisa katoliki  Parokia ya Mpwapwa jimbo kuu la
Dodoma,wameaswa    kuwahurumia na kuwasaidia wahitaji katika kipindi hiki cha kwaresma  na mwaka  wa huruma ya mungu  ili kuweza kujipatia Baraka na rehema za mungu.

Kauli hiyo imetolewa na Padre Daud Ngimba Paroko wa parokia ya Mpwapwa alipokuwa  akiongea  na radio mwangaza fm  kwa mahojiano maluum juu ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Kwaresma.

Padre Ngimba amesema mama kanisa katika kipindi hiki cha kwaresma  anawataka waumini   kuwasaidia wahitaji zaidi, kuwafariji  wanyonge  pamoja na kuwatembelea  makundi yaliyotengwa na jamii kama wafugwa na vituo vya watoto  yatima na vikongwe.

Akizungumzia  mwaka wa huruma ya mungu Padre Ngimba amesema  kuwa waamini lazima  wawe karibu na skarament ya kitubio,kasali kwa nia za baba mtakatifu   na kutimiza masharti  yote yanayo endana na huruma ya mungu ili kuweza kujipatia rehema kamili.

Aidha Pd Ngimba    amewataka  waamini  kusali  kwa nia ya
kuombea uchaguzi mkuu ndani ya kanisa Parokiani Mpwapwa  ili  kupata viongozi watakaolisaidia kanisa kusonga mbele na kuondoa chanagamoto zinazo likumba kanisa kwa sasa.
NGOI/SL                                       MWISHO.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree