Serikali imemnyany’anya mwekezaji wa
kampuni ya Via Avition karakana ya kutengeneza na kutunza ndege iliyopo
kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na kuirudisha kwa
shirika la ndege ATCL kutokana na mwekezaji kulipa ushuru mdogo wa dola
elfu tatu kwa mwezi huku yeye akiingiza malioni ya fedha hali iliyotajwa
kuwa ni kuitia serikali hasara na ufujaji wa rasimali za Umma.
Akitoa maamuzi hayo waziri wa ujenzi mawasiliano na uchukuzi Prof
Makame Mbarawa aliyetembelea uwanja huo na miradi mingine ya wizara yake
kukagua utendaji wa kazi amesema serikali imefika hatua hiyo baada ya
mwekezaji kupewa miaka kumi ya uendeshaji wa karakara hiyo lakini
amekuwa akilipa fedha kidogo na kuitia hasara serikali hiyo imeichuka na
kuirudisha serikali kwani hakuna muda wa kufumbia macho hujuma za
rasimali za umma.
Akizungumzia maamuzi hayo mwekezaji wa kampuni ya Via Aviation
Suzani Machibe amesema kwakuwa shirika la ndege Tanzania ATCL halina
uwezo wa kujiendesha kutoka na na uchache wa ndege zake walitumia
karakara hiyo kwa matengenezo ya ndege ya mshirika mengine hivyo
ameiomba serikali kutonyanyang’anya na badala yake waingine naye ubia
kuendesha karakana hiyo.
Kaimu mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro Bakari Murusuru
amesema watatekeleza maagizo ya serkali ikiwamo kukabiliana tatizo la
upitwishaji wa dawa za kulevya pamoja na utoroshwaji wa nyara za serkali
kwa kuimarisha ulinzi pamoja na kuweka mitambo ya kisasa katika uwanja
huo.
Post a Comment