SERIKALI imeahidi kuendelea kufanya tathimini katika maeneo yote nchini yaliyokumbwa na ukame ili ione namna ya kuwasaidia wahanga.
Ahadi
hiyo imetolewa leo bungeni mjini Dodoma na waziri wa nchi ofisi ya
waziri mkuu sera,bunge,kazi,ajira na walemavu mheshimiwa JENISTA
MUHAGAMA wakati akijibuswali la nyongeza la mbunge wa viti maalum
mhesmiwa FELISTER BURA aliyetaka kujua kama serikali ipo tayari
kushirikiana na wabunge kutatua majanga waliyopata wananchi kutokana na
mafuriko hasa katika mkoa wa Dodoma.
Mheshimiwa
MUHAGAMA amesema katika kipindi hiki nchi imekumbwa na mabadiliko ya
tabia ya nchi na kusababisha majanga yaliyotokea katika maeneo
mbalimbali nchini hivyo kama serikali watahakikisha wanaendelea na
tathimini.
Amesema kwa sasa inaziagiza kamati
za maafa kuanzia ngazi ya wilaya na mikoa kufanya kile kinachowezekana
kwa ngazi yao na yasiyowezekana yapelekwe serikali kuu.
.
MWISHO
SERIKALI
imeahidi kufanya tathimini ya uhaba wa chakula uliowakumba wananchi
katika maeneo mbalimbali nchini kwa dhamira ya kutoa chakula kwa haraka
ili kunusuru kaya husika.
Naibu
waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,kazi,ajira na walemavu
dr ABDALLAH POSSI amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu
swali la nyongeza la mbunge wa Mpwapwa GEORGE LUBELEJE.
Katika
swali lake mheshimiwa LUBELEJE ametaka kujua mpango wa serikali uliopo
wa kuwapatia chakula wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa na Kongwa ili waweze
kuepukana na njaa.
Dr
POSSI amesema serikali ina dhamira ya dhati ya kuwapatia wananchi wote
waliokumbwa na baa la njaa na mara baada ya tathimini kukamilika chakula
kitapatikana kwa haraka.
Awali
katika swali la msingi mheshimiwa LUBELEJE ametaka kujua mpango wa
serikali uliopo wa kuanza kugawa chakula cha njaa wilaya ya Mpwapwa
mkoani Dodoma.
Aijibu
swali hilo dr POSSI amesema kuanzia mwezi disemba mwaka jana hadi
januari mwaka huu jumla ya tani za chakula elfu 1,819 zimetolewa katika
wilaya hiyo na kutoa wito kwa wananchi waliopo katika maeneo ya ukame
kuhakikisha wanalima mazao yanayostahmili ukame na kufuata kanuni bora
za kilimo.
MWISHO
SERIKALI ya awamu ya tano imeahidi kuhakikisha wananchi wanapata maji kwa asilimia mia moja.
Waziri
wa maji injinia GERSON LWENGE ametoa ahadi hiyo leo bungeni mjini
Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Momba mheshimiwa
DAVID SILINDE aliyetaka kujua lini serikali itatekeleza sera ya Taifa ya
upatikanaji maji nchini ya mwaka 2002.
Injiinia
LWENGE amesema sera ya maji ya mwaka 2002 inatamka wazi kuwa umbali wa
upatikanaji wa maji uwe mita mia 4 jambo ambalo serikali imeshaanza
kutekeleza toka mwaka 2007 katika awamu ya kwanza ya mpango huo ingawa
bado hawajafikia lengo hivyo wataendeleza katika awamu ya pili ya mpango
huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Amesema Rais, Dr, JOHN MAGUFULI katika kampeni zake aliahidi upatikanaji wa maji na katika awamu hii maji itakuwa ni ajenda ya kwanza.
Katika
hatua nyingine serikali imesema italeta wazo la kuvuna maji ya mvua
katika awamu ya pili ya mpango wa upatikanaji wa maji unaotarajiwa
kuanza hivi karibuni na kuzitaka halmashauri zote nchini kuwa na mpango
wa kujenga mabwawa madogo madogo waliyo na uwezo nao ili kuhakikisha
madhara yatokanayo na mvua yanaepukwa.
Aidha, amesema serikali itaendelea kusimamia miradi mikubwa ya maji iliyoko nchi nzima na kuhakikisha inakamilika.
Injinia
LWENGE amesema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Hai na kiongozi
wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mheshimiwa FREEMAN MBOWE aliyetaka
kujua kwa nini serikali isiweke mpango maalum kupitia halmashauri wa
kuangalia namna ya kuhifadhi maji ili yasilete maafa na kuwezesha pia
kutumika katika kilimo.
Post a Comment