Taasisi isiyo ya
kiserikali “Broad Based Intersect Organization” (BBIO) ambayo inaratibu uhamasishaji
na uimarishaji wa mikakati ya maendeleo, yenye makao makuu mjini Dodoma imetambulisha
tuzo mpya ziitwazo AMAN Awards katika tasnia za muziki, filamu na habari.
Tuzo hizo zimetambulishwa
leo, jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo Aman Joram Mgullo.
Mgullo alisema kuwa, tuzo
hizo zimetokana na mradi uitwao “Advocacy Mission Awards Network” (AMAN) unaohusika
na uhamasisha na uimarishaji wa juhudi za utekelezaji wa mikakati ya maendeleo
“Wazo la utoaji wa tuzo
za AMAN limekuja baada ya Tanzania pamoja na mataifa mengine ulimwenguni kuzindua
mkakati mpya wa maendeleo (the Agenda 2030 of Sustainable Development Goals) ikiwa
na adhima ya kutengeneza Maisha bora na Dunia bora kwa kila mwanadamu
ulimwenguni,” alisema Mgullo.
Mgullo aliongeza kwa kusema
kuwa, kutokana na mikakati mingi iliyotangulia kutofanikiwa kufikia malengo
yake na kufanya jamii nyingi kuendelea kuishi katika hali duni ndicho
kilichopelekea taasisi ya BBIO kufanya juhudi za ushawishi na uwezeshaji kupitia
wasanii na wanahabari ili mradi huo wa maendeleo ufikie malengo yake kupitia tuzo
za AMAN.
Kutokana na tafiti
nyingi kuthibitisha kuwa tasnia za muziki na filamu, kupitia vyombo vya habari
zinauwezo mkubwa wa ushawishi na uwezeshaji kwa jamii. Hivyo kwa kuwashilikisha
wasanii kutoa ujumbe wa maendeleo kwa jamii kupitia tuzo za AMAN kutaleta
mabadiliko kwa jamii ya Tanzania.
Mgulla alizitaja tuzo
zitakazowaniwa kuwa ni Aman Music Awards, Aman Film Awards na Aman Media Awards
ndani ya kila Tuzo kutakuwa na vipengele tofauti tofauti, na wananchi watashiriki
kwa kupigia kura na kuchagua msanii au mwanahabari ambaye amefikisha ujumbe wa
maendeleo katika jamii.
Lengo la tuzo za AMAN
ni kuhakikisha dhima ya maisha bora na dunia kwa kila mwanadamu kwa kuchochea
umahiri katika kutoa, kueneza na kufikisha ujumbe wa maendeleo endelevu kupitia
tasnia za muziki, filamu na habari.
Post a Comment