BREAKING NEWS

Tuesday, 26 January 2016

Rais wa Iran kukutana na Papa Francis

Rouhani
Rais wa Iran Hassan Rouhani, amepangiwa kukutana na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis mjini Vatican leo.
Mkutano huo ni sehemu ya ziara ya kiongozi huyo wa Iran barani Ulaya ambayo inalenga kuimarisha uhusiano kati ya Iran na nchi za Magharibi.
Hii inajiri baada ya mataifa hayo kuiondolea vikwazo Iran.
Bw Rouhani alianza ziara yake Jumatatu, ambapo maafisa wa Iran walitia saini mikataba ya kawi na miundo msingi ya thamani ya dola bilioni 17 za Kimarekani kati ya Iran na kampuni za Italia.
Kutoka Rome, Bw Rouhani ataelekea Paris, ambako anatarajiwa kukamilisha mkataba na kampuni ya Airbus. Mkataba huo unahusu mpango wa Iran kununua zaidi ya ndege 100 kutoka kwa kampuni hiyo ya Ufaransa.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree