Mwendesha mashtaka mkuu nchini
Malaysia amemuondolea waziri mkuu wa taifa hilo Najib Razak tuhuma za
ulaji rushwa ambazo zilikuwa zimetikisa siasa nchini humo.
Afisa
ya mwanasheria mkuu imesema $681m (£479m) ambazo Najib alipokea kwenye
akaunti yake ya benki zilikuwa “mchango wa hisani wa kibinafsi” kutoka
kwa familia ya kifalme ya Saudi Arabia.Wapinzani wake walikuwa wamedai pesa hizo zlitoka wa mfuko wa uwekezaji wa serikali wa 1MDB.
Bw Najib amekuwa akikanusha tuhuma hizo lakini alikuwa amekabiliwa na shinikizo za kumtaka ajiuzulu.
Maafisa wa kupambana na rushwa walikuwa awali wamesema alipokea pesa hizo kutoka kwa mfadhili wan je ya nchi.
Mwanasheria mkuu Mohamed Apandi Ali amesema kupitia taarifa kwamba pesa hizo zilitoka kwa familia hiyo ya kifalme ya Saudia na zilitumwa kwenye akaunti yake ya benki mwishoni mwa Machi au mapema Aprili 2013.
Ameongeza kwamba maafisa wa kupambana na rushwa wamekutana na mashahidi, akiwemo mtu aliyetambuliwa kama “aliyetuma pesa hizo” kuthibitisha habari hizo.
“Nimeridhika kwamba hakuna ushahidi pesa hizo zilikuwa rushwa,” amesema.
Post a Comment