BREAKING NEWS

Tuesday, 26 January 2016

Wanajeshi wa Kenya 'waondoka el-Adde'


 Somalia


Wakazi kusini mwa Somalia wanasema majeshi ya Kenya yameanza kuondoka kutoka eneo la el-Adde ambako kambi ya majeshi hayo ilishambuliwa wiki moja iliyopita.
Ripoti zinasema wanajeshi hao wameondoka el-Adde pamoja na miji mingine ya karibu.
Msemaji wa majeshi ya Kenya Kanali David Obonyo hata hivyo amesema kuondoka kwa wanajeshi hao ni jambo la kawaida.
Wanajeshi karibu 4,000 wamekuwa wakihudumu chini ya majeshi ya Muungano wa Afrika (Amisom) kuisaidia serikali ya nchi hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na tishio kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab.
Wakazi wamekuwa wakilalamikia kunyanyaswa na wanajeshi wa Kenya tangu kushambuliwa kwa kambi hiyo tarehe 15 Januari, na wamefurahia kuondoka kwa wanajeshi hao.
Kanali Obonyo amesema kuondoka kwa wanajeshi hao ni moja moja tu ya mipango ya kijeshi na hakufai kutazamwa kama kuondoka kabisa kwa wanajeshi eneo hilo.
Al-Shabab wanasema waliwaua wanajeshi zaidi ya 100 baada ya kushambulia el-Adde.
Serikali ya Kenya imepuuzilia mbali habari hizo ingawa bado haijatoa takwimu rasmi ya wanajeshi waliouawa au kujeruhiwa.
 

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree