Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala yapiga marufuku uuzwaji holela wa bidhaa katika
soko la Buguruni unaochafua mazingira ya soko na kuhatarisha afya za
walaji.
Hayo
yamesemwa leo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala David
Langa wakati akifafanua kuhusu kero ya wauzaji holela wanaopanga bidhaa
chini katika soko la Buguruni.
“Bidhaa
zinazopangwa chini katika soko la Buguruni sio rasmi na hakuna utaratibu
unaoruhusu wauzaji kufanya biashara hiyo, hivyo natoa tahadhari kwa
wale wote wenye tabia hiyo kuwa ni marufuku kufanya biashara ya kupanga
bidhaa chini na sio kwa soko la Buguruni tu ila katika masoko yote
yaliyopo katika manispaa yetu” Alisema Langa.
Afisa
langa amesema kuwa wapo maaskari wanaolinda na kuthibiti uuzwaji holela
wa bidhaa katika soko hilo ila wauzaji wamekuwa wakifanya mchezo wa
kuwavizia maaskari pindi wanapoondoka ndipo wanapanga bidhaa zao.
Ameongeza
kuwa suala hili limekuwa sugu katika masoko mengi na njia ya
kukabiliana na changamoto hii ni kuongeza askari wengi watakaokaa muda
wote ili waweze kukabiliana na wauzaji holela.
Aidha
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Maafisa Afya
inafatilia kwa karibu masoko yote ili kufatilia kama wauzaji
wanazingatia kanuni za afya kwa kuweka mazingira safi ili kuokoa afya za
walaji.
Uchafu wa
mazingira katika masoko ya Jiji la Dar es Salaam umekithiri na imekuwa
ni tatizo sugu lakini Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imejipanga
kupambana nalo ili kuondoa uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko
kama kipindupindu
Post a Comment