Wazazi na
Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika
Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza,
wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze
kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.
Wazazi
hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika kwa kikao baina yao
na uongozi wa Shule hiyo pamoja na Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima
Mkoani Mwanza, sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya
Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.
Malalamiko
yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu awali kuwa watoto wao
wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa
na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.
Awali
wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada kwa ajili ya watoto
wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo lililomlazimu Malimi Joram ambae
ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani
Mwanza kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima
hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa kuwa Serikali haitoi
ruzuku kwa ajili yao.
Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela.
Wakati
ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo
ya Pasiansi akasisitiza suala la wao kuondolewa ada ili nao wanufaike
na mpango wa elimu bure.
Kitengo
cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya Sekondari Pasiansi,
kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa
la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo
la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango
mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu
Hamsini kwa mwaka.Kikao Kikiendelea
Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa
Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi
juu ya suala la Elimu Bure nchini.(P.T)
Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza
Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi
Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa
kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
Post a Comment