Tuesday, 26 January 2016
Madhabahu ya Mama Yetu wa Rozari ya Fatima, kufunguliwa upya
Posted by Unknown on 12:02:00 in | Comments : 0
Gombera wa Madhabahu ya Mama yetu wa Rozari ya Fatima Ureno, ametangaza habari njema ya kukamilika kwa kazi za ukarabati na marekebisho, zilizokuwa zikifanyika katika Madhabahu ya Mama Yetu wa a Rozari ya Fatima Ureno, kwamba Madhabahu hayo, yatafunguliwa upya rasmi hapo tarehe Februari 2, wakati wa adhimisho la Siku kuu ya Bwana kutolewa Hekaluni, sanjari na Siku ya Watawa Duniani.
Padre Carlos Cabecinhas , ameviambia vyombo vya habari kwamba, ukarabati uliofanyika ni kwa manufaa ya waamini wanatakao penda kutoa heshima zao na kusali katika makaburi ya Wenye Heri Francisco na Jacinta Marto yaliyoko karibu madhabahu kuu . Kwamba , kwa sasa njia inayokwenda kwenye makaburi ya wachungaji wadogo waliotokewa na Mama Maria, ambayo awali ilikuwa ikichanganya mahujaji, kwa sada imewekwa wazi zaidi na hivyo ni rahisi kufika katika makaburi hayo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Katoliki SIR, Askofu wa Leiria-Fatima, António Marto, ataongoza Ibada ya Misa kwa nia ya kutabaruki madhabahu mapya , hapo tarfehe 2 Februari 16, ya Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Rozari wa Fatima. Padre Cabecinhas ameendelea kueleza kwamba, baada ya kufunguliwa kwa Basilika la Mama Yetu wa Fatima, Ibada za Misa zitakuwa zikisomwa kila siku kwa mahujaji .
Kazi ya Michoro ya sasa katika Madhab ahu imefanywa na msanii maarufu Bruno Marques kwenye Basilka hilo ambalo ujenzi wake ni ulianza mwaka 1928, kwa michoro ya mtalaam wa majengo wa Uholanzi, Gerard Van Kriechen na kujengwa na mhandisi wa Ureno João Antunes. Jengo hilo lililowekwa Wakfu Oktoba 7, 1953, lina urefu wa mita 70.5 na mapana ya mita 37, na liliwekwa wakfu kwa Mama yetu wa Rozari na Papa Pius XII, kwa hati yake ya Kipapa ya "Luce Superna" ya Novemba 11, 1954.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment