Tuesday, 26 January 2016
Papa Francisko ahimiza Wakristo kutembea njia ya Umoja
Posted by Unknown on 11:59:00 in | Comments : 0
Jumanne jioni akiongoza Ibada ya Maombi katika Kanisa la Mtakatifu Petro nje ya Kuta mjini Roma, Papa Francisko, alihimiza Wakristo kutembea katika njia ya huruma na msamaha, kusahau makosa ya nyuma na badala yake wasonge mbele kwa pamoja katika njia ya umoja. Aliomba kutoruhusu makosa ya nyuma kuendelea kuchafua uhusiano kati ya Wakristo. Papa alieleza hilo wakati akiongoza sala za jioni, kwa nia ya kuhitimisha Wiki la Kuombea Umoja wa Wakristo, ambalo kila mwaka huanza tarehe 18 -25 Januari.
Katika hotuba yake, Baba Mtakatifu alilenga zaidi katika haja ya jumuiya za Kikristo zilizotengana, kujenga umoja na kutembea pamoja katika njia ya Bwana kwa utambuzi kwamba, umoja ni zawadi toka mbinguni na katika uelewa kwamba, huduma zote zinazotolewa katika jina la Injili ni kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa moja la Kweli kwa utukufu wa Bwana mmoja, Yesu Kristo.
Baba Mtakatifu alieleza na kupendekeza kwamba ”wakati wa safari hii ya pamoja kuelekea ushirika kamili, kunaweza anzishwa mwendelezo wa aina nyingi za ushirikiano, katika neema kueneza Injili - na katika kutembea pamoja kwa utambuzi kwamba, tayari tumeungana katika jina la Bwana."
Baba Mtakatifu aliendelea kutafakari umoja wa Wakristo akiangalisha pia katika uwepo wa Maadhimisho ya Jubilee ya Mwaka Mtakatifu, akisema yeye kama Askofu wa Roma, alipenda kuomba msahama kwa niaba ya Wakatoliki kwa utendaji wa Wakatoliki, ulioumiza Wakristo wa makanisa mengine, kinyume na maadili ya Injili. Na wakati huo huo, akawaomba Wakatoliki wote kusamehe makosa yaliyofanywa na Wakristo wa madehebu mengine dhidi yao, iwe nyakati hizi au siku za nyuma . Alikumbusha katika Maadhimisho ya Jubilee hii maalum ya Mwaka Mtakatifu wa kuomba Huruma ya Mungu , ni lazima daima kukumbuka kwamba, hapawezi kuwa na mchakato wa kweli wa kujenga Umoja wa Wakristo bila kutegemea kikamilifu huruma ya Baba. Na kwamba ni tu huruma ya Mungu, inayoweza kujenga uhusiano mpya kati ya Wakristo.
Baba Mtakatifu alieleza hayo mbele ya umati mkubwa wa waamini wakiwemo wawakilishi kutoka makanisa mengine na jumuiya , waliohudhuria Ibada hiyo kwa ajili ya kukamilisha Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo. Kati yao, alikuwepo Mwakilishi kutoka Kansia la Kiotodosi Askofu Mkuu wa Gennadionsi aliyewakilisha Upatriaki wa Kiekumeni , na Askofu Mkuu David Moxon wa Kanisa la Kianglikan. Mwanzo wa Ibada Papa aliwaalika wajiunge nae kutembea pamoja kupita Mlango Mtakatifu wa Kanisa la Mtakatifu Paulo nje ya kuta. Papa Francisko amesisitiza kwamba , inawezekana kufanya maendeleo katika njia wazi za ushirika kamili, si tu wakati wa mikutano au wakati kunapokuwa na haja ya kukutana ana kwa ana , lakini juu ya yote, kupitia uongofu aminifu wenye kutuweka karibu zaidi na Bwana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment