Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bituni
Msangi amewaagiza Viongozi wa Vijiji na Mitaa kuwakamata Wananchi wanaotumia vibaya fedha za Tasaf awamu ya tatu wa kunusuru kaya maskini
hapa Nchini.
Mkuu huyo wa Wilaya aAametoa kauli
hiyo jana kwa nyakati tofauti alipofanya
ziara ya kutembelea baadhi ya Vijiji kuangalia zoezi la ulipaji ruzuku ya fedha za Tasaf kwa Walengwa wa mapango huo wenye lengo la kuzinusuru Kaya maskini.
Msangi amewaagiza Viongozi hao kuwafuatilia na
kuwakamata wale wanaotumia vibaya fedha za mpango wa Tasaf kinyume na malengo ya Serikali ya kuzinusuru
kaya hizo ambazo ni maskini .
“Ninawaagiza Watendaji wote wa mitaa
na Vijiji kuwakamata mara moja Wananchi wale wanaotumia vibaya fedha za Tasaf kwa
kuzinywea Pombe na kufanya maisha ya anasa, wapelekwe mahakani maana wanahujumu
nia njema ya Serikali ya kuwatoa kwenye umaskini”alisema.
Alisema Fedha hizo zinatolewa na Tasaf
ili kuzikwamua Kaya maskini kwa kuongeza
kipato na kuondoka kwenye lindi la umaskini ambapo awali
Familia hizo walishindwa hata kupata mlo moja kwa siku.
Masangi alisema sehemu ya fedha hizo
za ruzuku itumike kununulia chakula cha familia hasa kipindi hichi cha njaa
ilitokana na ukame kwa miaka miwili iliyopita.
Aidha aliwashauri kubuni miradi
midogomidogo kutokana na ruzuku hiyo wanayopatiwa ili kuwasaidia baadaye wakati
wa ikomo wa mradi huo utakapofika kwa sababu mapango huo ni wa muda maalumu.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Kongwa White Zuberi alisema kutokana Serikali kuanza kutoa elimu bure Wazazi hao wamesaidiwa
kuepuka michango ambayo kipindi cha nyuma walitumia sehemu ya ruzuku hiyo
kulipa ada za shule.
Amewawataka wasiishie kuwanunulia
mahitaji peke yake pia wahakikishe wanafuatilia maendeleo ya Watoto wao katika shule wanazosoma ili kujua kama wanafika
huko na baada ya kurudi wakague
madaftari yao .
Kwa upande wake mratibu wa Tasaf
Wilaya ya Kongwa Magesa Makaranga amesema tangua kuanzishwa kwa mpango huo wa kunusuru
kaya Maskini Nchini mwaka 2014 Tasaf
Wilaya hiyo inatekeleza mpango huo katika
vijiji 43 na malipo hayo ni ya awamu ya tisa.
Makaranga amesema kaya 8455
zimenufaika na mapango huo na mpaka januari mwaka huu na wameshawalipa Walengwa zaidi ya shilingi
bilioni 2.8 tangu kuanza kwa mradi huo.
Mwisho.
Post a Comment