Mtoto
wa miaka 11, Nchambi Tungu, ameuawa kikatili na mama yake mzazi kwa
kuchapwa fimbo kisha kumfunga kamba shingoni na kumning’iniza kwenye
tawi la mwembe ili ionekane kuwa amejinyonga mwenyewe.
Inaelezwa
kuwa mama wa mtoto huyo, Sado Roketi (26) mkazi wa kitongoji cha
Mnyakasi, kijijini Ikuba, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi alimuua mwanawe
huyo baada ya kukataa kumfulia nguo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Alisema
tukio hilo ni la Januari 23, mwaka huu saa moja jioni katika Kitongoji
cha Mnyakasi. Alisema siku ya tukio mtuhumiwa alimpatia mwanawe huyo
nguo amfulie lakini mtoto huyo alikataa kuzifua akaendelea kucheza na
wenzake.
“Ndipo
mama huyo kwa hasira alipoamua kuchukua fimbo na kuanza kumpiga sehemu
mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo, aliubeba mwili na
kuutundika kwenye matawi ya mti wa mwembe baada ya kumfunga kamba
shingoni na kumwacha akining`inia ili ionekane alijinyonga mwenyewe,” alieleza Kidavashari .
Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Post a Comment