WILAYA
ya Ulanga iliyopo Mkoani Morogoro imefanikiwa
kupunguza matukio ya kesi
za mimba mashuleni kwa wanafunzi wanaosoma shule za sekondari na Msingi
wilayani humo, kutoka mimba 81 kwa mwaka 2014 hadi kufikia mimba 28 kwa
mwaka 2015 huku kwa upande wa Msingi ikipunguza mimba 3 kwa 2014 hadi kufikia 0
kwa mwaka 2015.
Hayo
yamebainishwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Christina Mndeme, ambapo alisema kuwa wilaya hiyo imedhamiria kabisa kufuta mimba
kwa wananfunzi wanaosoma shule za sekondari Wilayani humo, na kwa mwaka huu
wameanza kwa kauli mbii inayosema “MAGAUNI MANNE” kauli ambayo kila
mwanafunzi anatakiwa kuhifahamu.
Mndeme
amesema kuwa m atukio ya kesi za mimba kutoka shule moja hadi nyingine
yamepungua kutokana na Wilaya hiyo kutumia kauli mbiu ya “NIACHE NISOME”
ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza hamasa ya mapambano dhidi ya mimba
kwa wanafunzi waliopo mashuleni.
Aidha
amesema kuwa kwa sasa wameanza kampeni
ya kuzunguka katika kila shule, na kufanya vikao vya pamoja baina yao na
wananfunzi wa kike, lengo likiwa kuwajena kisaikolojia, na kuwafundisha namna
ya kujiepusha na wananume wakware, ambao wamekuwa wakiwapatia ujauzito, na
kupelekea kukatisha masomo yao.
Baadhi
ya wanafunzi waliokatisha masomo yao kutokana na kupewa ujauzito, wamesema kuwa wanajisikia uchungu kuona wamesitisha ndoto
zao za kuendelea na msomo, hivyo wamewaomba wanafunzi wanaoendelea
na masomo, kuwa makini na kuepukana na vishawishi ambavyo vinaweza kuwaingiza
katika mambo ya anasa na matokeo yake kuishia kupata ujauzito.
Hata
hivyo Serikali ya Wilaya hiyo imesema kwa sasa imeweka mikakati ya kukabiliana
na tatizo hilo, kwa kuanzisha msako kwa wananume wote ambao wamekuwa wakijihusisha
na mapenzi kwa wanafunzi wa sekondari, kumalizia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi
wa kike pamoja na kuendelea kutoa elimu kupitia radio na televisheni juu ya
athari zinazoweza kuwapata wanafunzi wa kike mara baada ya kukatisha masomo yao
kutokana na ujauzito.
Post a Comment