BREAKING NEWS

Wednesday, 27 January 2016

Mwenyekiti kijiji cha Matongoro Wilayani Kongwa auza Chakula cha msaada

BAADHI ya wakazi wa Kijiji cha Matongoro wilayani Kongwa mkoani dodoma wamelalamikia kitendo cha mwenyekiti wa kijiji hicho Moses Daudi kuuza chakula cha msaada ilihali wao wanakabiliwa na njaa.

Wakizungumza na a wapo redio kijijini hapo wakazi hao walidai kuwa kitendo hicho ni cha kifisadi kwa viongozi wa serikali ya kijiji kuingiwa na tamaa hivyo ni vyema wakachukuliwa hatua za kisheria.

Mmoja wa wakazi hao Ndonye Chedego alisema kuwa walipata taarifa ya kuwepo kwa chakula cha msaada gunia 59 ambazo zilipelekwa kijijini kwaajili ya vikongwe na walemavu .

Alisema kuwa Kamati ya maafa ilishirikishwa kuhusiana na kuletwa kwa chakula hicho ndipo chakula kikaanza kugawiwa juzi asubuhi kwa watu ambao walishapata chakula hicho awamu iliyopita.

Utaratibu wa ugawaji wa chakula cha msaada hapa kijijini kwetu ulikiukwa lakini jambo la kushangaza ni baada ya kuwabaini watu wana magunia ya mahindi kitu ambacho kilitushtua sana.

Aidha aliema kuwa walishangaa kukuta baadhi ya wakazi wenzao wakiwa na  magunia ya mahindi ndipo wakawabana wakazi hao na kueleza kuwa wameuziwa na Mwenyekiti wa kijiji pamoja na mtendaji.

Kwakweli tunaiomba Serikali iingilie kati suala hili  kwani tumekuwa tunateseka na njaa na hatuna uwezo

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho,Moses Daud alipoulizwa kuhusiana na suala hilo la kutuhumiwa kuuza chakula cha msaada alikataa kuwa sio kweli bali mtendaji aliuza mahindi gunia nne tu kwakushirikiana na kamati ya maafa  ili kulipia nauli ya gari ambayo ilibeba mahindi hayo.
kwa upande wake mkulugenzi mtendajiwa wa halimashauri ya wilaya ya kongwa amesema hawezi kuongea na mwandishiwa habari  kwa njia ya simu hadi afike ofisini kwake.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree