Moto
mkubwa umeteketeza hoteli ya kitalii ya Konokono Beach Resort iliyoko
Michamvi mkoa wa kusini Unguja, inayomilikiwa na mtoto wa rais wa zamani
wa Zanzibar, Amina Karume pamoja na wawekezaji wawili kutoka nje ya
nchi.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Kusini Unguja, Juma Saadi amesema kuwa moto huo
uliteketeza nyumba tatu na mgahawa mmoja katika hoteli hiyo, ni watu
wawili waliokuwa wakichoma nyasi karibu na hotel hiyo. Aliwataja vijana
hao kuwa ni Meshak Amos Elisha na Mohamed Abdallah Hassan.
Kamanda
Saadi aliwataka wananchi kupuuza habari zilizoenea zinazohusisha tukio
hilo na mambo ya kisiasa, husasan vyombo vya habari vya kimataifa
vilivyoripoti habari hiyo.
“Wakati
wa kuchoma moto ndani ya uzio huo, ulizuka upepo mkali majira ya saa
tano na nusu na kusababisha nyumba moja ya makuti katika hoteli ile
kushika moto na kusababisha hasara hiyo,” kamanda Saadi alifafanua.
Kikosi cha zima moto na uokoaji kilifika katika eneo hilo na kufanya kazi za kuzima moto huo.
Post a Comment