Mtu wangu wa nguvu najua imekuwa kawaida
kwa kila staa kuweka style ya nywele katika muonekano tofauti tofauti,
hususani katika muonekano ambao sio wa kawaida, yaani haujazoeleka
machoni mwa watu. Hadi kufikia August 2014 hii ndio ilikuwa TOP 10 ya
style mbaya za nywele kwa mastaa wa soka.
10- Raheem Sterling alikuwa katika hii
list ila wakati huo akiwa katika klabu ya Liverpool ya Uingereza,
Sterling kwa sasa anaichezea klabu ya Man City.9- David James ni golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na
vilabu vya Liverpool na Manchester City, style yake ya nywele iliingia
kwenye headlines hizi.8- Rene Higuita ni golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Colombia,
ukiachana na style yake ya nywele kuwahi kuingia katika list ya style
mbaya za nywele, anajulikana kwa style yake “scorpion kick” ya uokoaji
mipira langoni.7- Namba saba haikuwa ikimilikiwa na mchezaji mmoja, ila mabeki watatu
ndio walipata nafasi ya kumiliki namba ya count down hii, kutokana na
style zao za nywele kufanana, David Luiz, Carles Puyol na Fabricio
Coloccini.6- Marouane Fellaini style yake ya nywele haitofautiani sana na style ya
nywele ya David Luiz, Carles Puyol na Fabricio Coloccini ila Fellaini
kapewa namba sita. Fellaini anatajwa kuwa huenda umahiri wake wa kupiga
sana mipira ya vichwa wakati akiwa Everton ulitokana na msaada wa nywele
zake.5- Ronaldo de Lima style yake ya nywele iliingia kwenye headlines katika
fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2002. Sababu ya Ronaldo
kunyoa hivyo ni kutokana na mtoto wake kushindwa kuwatofautisha na
Roberto Carlos wakati wanacheza mpira akiwaangalia kwenye TV.4- Giovanni Simeone huyu ni mtoto wa kocha wa sasa wa Atletico Madrid
Diego Simeone ambaye style yake ya nywele haikuishia kutajwa kuwa ni
style mbaya pekee, ila inawezekana ikawa ni style mbaya kuwahi kutokea
katika historia ya soka.3- Djibril Cisse jamaa aliwahi kutamba na timu ya taifa ya Ufaransa na
klabu ya Liverpool kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2007, Cisse amekuwa
akijulikana kwa kupenda kubadili mitindo ya nywele kichwani, kitu
ambacho kilimfanya pia kuwa maarufu ukiachana na uwezo wake uwanjani.2- Chris Waddle kwa Uingereza hii ilikuwa moja kati ya style za nywele
zilizowahi kuwekwa nakutamba licha ya kuwa zipo katika count down ya
stori 10 mbaya, Waddle alikuwa kiweka mtindo huo wa nywele wakati akiwa
Tottenham Hotspurs.1- Taribo West katika count down hii huyu ndio staa pekee kutoka Afrika
aliyeingia kwenye hii count down, staa huyo wa kimataifa wa Nigeria
ambaye alistaafu kucheza soka miaka kadhaa nyuma, ndio alikuwa katika
rekodi ya kuwa na style mbaya ya nywele kuliko wote.
Post a Comment