Alisema, hiyo ndiyo dhamira ya Yesu, na utume wa Kanisa, kuhubiri habari njema kwa maskini. Na kwamba, ingawa Habari Njema inahubiriwa kwa watu wote , Papa alielezea, Yesu anatoa kipaumbele zaidi kwa wale waliombali nae, walio katika mateso, wagonjwa na walio telekezwa na jamii kutokana na hali yao duni kimaisha. Aliwataja Maskini, hasa ndio walengwa katika Injili.
Baba Mtakatifu Francisko aliendelea kueleza nini maana ya kutangaza kwa maskini habari njema. Alisema zaidi ya yote, ina maana kuwa karibu na maskini, kuwatumikia kwa furaha , kuwapa habari ya kukomboa dhidi ya ukandamizaji. Yote hayo, yakifanyika katika jina na Roho wa Kristo, kwa sababu Yesu ndiye Injili ya Mungu mwenyewe, Yeye ni Huruma ya Mungu, Yeye ni ukombozi wa Mungu. Baba Mtakatifu alieleza na kuhoji iwapo kazi za uinjilishaji katika parokia hutoa kipaumbele kwa maskini zaidi katika Parokia, na iwapo hiyo ndiyo azma kuu kwa vyama na jumuiya za Kanisa. Na iwapo waamini ni aminifu katika mpango huo wa Kristo?
Aliweka bayana kwamba , kupeleka habari njema kwa maskiini haina maana tu kutoa msaada wa kijamii au kisiasa, lakini inahusu kutenda kwa nguvu ya Injili ya Mungu, yenye kuleta wongofu mioyoni , kuponya waliojeruhiwa na kufanya mageuzi mazuri katika uhusiano wa kijamii kwa mujibu wa mantiki ya upendo
Baba Mtakatifu alikamilisha hotuba yake kwa kuomba msaada wa Mama Bikira Maria, Mama wa Waenezaji Injili, awasaidie wote kupata hamu na kiu ya kutaka kueneza Injili duniani kote, na hasa kuifikisha Injili katika mioyo ya maskini wengi wa kiroho , na kumwezesha kila mmoja na kila muumini na jumuiya nzima ya kikristo, kuwa shahidi imara wa huruma ya Mungu, ambayo hutoka kwa Kristo.
Post a Comment