BREAKING NEWS

Tuesday, 26 January 2016

Marais wa Iran, Italia wafanya mazungumzo Roma



Marais wa Iran, Italia wafanya mazungumzo Roma

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yuko mjini Roma Italia alikowasili leo na kulakiwa rasmi na rais wa nchi hiyo.
Baada ya Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwasili nchini Italia leo, amelakiwa na Rais Sergio Mattarella wa wa nchi hiyo katika ikulu ya rais.
Katika mahojiano na mwandishi wa Radio Tehran mjini Roma, Mohammad Nahavandian, Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Iran amesema kuwa mazungumzo ya maraia hao wawili yalikuwa mazuri.
Amesema katika mazungumzo ya marais Rouhani na Mattarella pande mbili zimejadili njia za kuimarishwa ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tehran na Roma.
Rais Hassan Rouhani akiongoza ujumbe wa ngazi za juu leo Jumatatu amewasili katika mji mkuu wa Italia na baada ya hapo anatazamiwa kuelekea katika nchi jirani ya Ufaransa.

Share this:

 
Back To Top
Distributed By Rodrick Minja | Designed By Bill De Pierree