Wakazi
wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wamempongeza Rais John Magufuli
kwa hatua aliyochukua ya kuahirisha maadhimisho ya siku ya Muungano na
kuokoa zaidi ya Sh bilioni mbili na kuagiza fedha hizo zitumike kufanya
upanuzi wa Barabara ya Ghana kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Pamoja
na pongezi hizo, wamemuomba Rais Magufuli baada ya barabara hiyo
kukamilika kufanyiwa upanuzi, ipewe jina la “Barabara ya Muungano” kama
njia ya kuienzi kauli yake hiyo aliyoitoa kwa wakazi wa jiji hilo.
Rais
Magufuli akiwa Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko, juzi
alitangaza kuahirisha maadhimisho ya siku ya Muungano mwaka huu na
kuagiza fedha ambazo zingetumika kwa vinywaji, halaiki, gwaride na
vyakula ambazo ni zaidi ya Sh bilioni mbili, zitumike kufanya upanuzi wa
Barabara ya Ghana – Airport.
Kadhalika alielekeza siku hiyo iwe siku ya mapumziko ya kawaida kwa Watanzania kuiadhimisha wakiwa katika shughuli zao binafsi.
<a
href='http://mpekuzihosting.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a5fa0220&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE'
target='_blank'><img alt='' border='0'
src='http://mpekuzihosting.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=3&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE&n=a5fa0220'/></a>
Post a Comment