Rais
Magufuli ametoa mchango wa shilingi milioni 10 kwa kanisa la bikira
Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita kwa ajili kuchagia upanuzi wa kanisa
hilo ambapo fedha hizo zimekabidhiwa na kaimu mnikulu Ngusa Samike
katika misa ya pili ya ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka, iliyofanyika
kanisani hapo leo tarehe 03 April, 2016.
Kabla
ya misa hiyo ya pili Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa
pamoja na Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga na Mkewe Mama Ida
Odinga, walisali misa ya kwanza ambapo Rais Magufuli aliahidi kuchangia
shilingi milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo ambao
unaendelea.
Taarifa
iliyotolewa na Ikulu imesema katika misa hiyo Paroko wa Parokia ya
Chato, Padre Henry Mulinganisa alieleza kuwa kanisa hilo linatarajia
kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake baadaye mwaka huu, na
kwamba maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na upanuzi wa kanisa ambao
unachangiwa na waumini wenyewe.
Padre
Mulinganisa amemshukuru Rais Magufuli kwa mchango huo na amemuahidi
kuwa utatumika vizuri ili uendeleze upanuzi wa kanisa hilo pamoja na
michango ya waumini wengine.
Post a Comment